Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumamosi, 2 Februari 2019

Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo. Ninazungumzia asili ya binadamu katika kila ushirika, kufikia chanzo, kuchanganua asili ya binadamu, na kuchanganua kiini. Ni juu yenu basi kuwasiliana ufahamu wenu kuhusu hizi mada.

Mnapaswa kuelewa kusudi la Mungu na ni lazima muijue asili ya binadamu kupitia hii miaka saba ya majaribu. Kwa hakika, kila sentensi ya Mungu ina kusudi Lake, ambamo mmefichwa ukweli. Bila kujali ni suala gani linafanyiwa ushirika, au ni ukweli gani unaoenyeshwa, ndani yake mna njia ambayo watu wanapaswa kupitia, matakwa ya Mungu kwa watu, na kusudi la Mungu kwa wanaomtafuta. Katika haya mazungumzo ya majaribu, dhiki, na hatimaye mateso, matakwa kwa watu na kusudi la Mungu pia vimo ndani. Watu, bila shaka, wanaonyesha hisia kwa mitazamo yao, kwa kuwa watu hawajaundwa kwa mbao; wako hai, na wanaonyesha hisia kwa kila kitu. Je, kuna maana kuchanganua ni hali gani za asili ya binadamu zinawakilishwa katika hisia za watu? Ina maana kushiriki kuihusu? Uchanganuzi utasaidia watu kuliona hilo wazi, kulijua wao wenyewe, na kujua vyema kabisa mioyoni mwao ili kwamba hatimaye wawe na njia mwafaka ya kuchagua. Ikiwa mtu amekanganyikiwa na hajui kusudi la Mungu, haelewi ukweli, na ana ufahamu mdogo kuhusu matakwa ya Mungu kwake na wajibu anaopaswa kutekeleza, au njia gani anapaswa kutembea, pengine mtu wa aina hii hatasimama imara. Kwa hivyo, inapaswa kujulikana ni njia gani inapaswa kutumiwa baadaye wakati wa majaribu mbalimbali.

Kila wakati majaribu ya miaka saba yanapotajwa, kuna watu wengi wanaohisi vibaya sana na kuvunjika moyo kusiko kwa kawida, na kuna watu wengine ambao hulalamika, na kuna mchanganyiko wa hisia. Ni dhahiri kutokana na hizi hisia kwamba watu sasa wanahitaji majaribu haya, wanahitaji aina hii ya dhiki na utakasaji. Watu humwamini Mungu kwa nia ya kutaka kupata baraka siku zijazo. Watu wote wana kusudi na tumaini hili. Hata hivyo, upotovu ndani ya asili ya binadamu ni lazima uondolewe kupit majaribu. Katika hali yoyote usiyoipita, ni katika hizi hali ambamo ni lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili ujue upotovu wako mwenyewe. Hatimaye unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu.

Hivyo ikiwa watu hawana miaka kadhaa ya usafishaji, ikiwa hawana kiwango fulani cha mateso, hawataweza kuepuka utumwa wa upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yao. Katika hali zozote zile bado ungali mtumwa wa Shetani, katika hali zozote bado ungali na tamaa zako mwenyewe, matakwa yako mwenyewe—ni katika hali hizi ambamo unapaswa kuteseka. Mafunzo yanaweza kupatikana tu katika mateso, yaani, kuweza kupata ukweli, na kuelewa kusudi la Mungu. Kwa kweli, ukweli mwingi unafahamika katika uzoefu wa majaribu makali. Hakuna asemaye kuwa kusudi la Mungu linajulikana, kwamba uweza na busara Yake vinafahamika, kwamba tabia ya haki ya Mungu inaonekana katika mazingira ya utulivu au katika hali zinazofaa. Hilo haliwezekani!

Mungu ametayarisha mazingira mwafaka ambamo Anawafanya watu kuwa wakamilifu, ila haijulikani kwa yeyote ni kwa nini Mungu anaweza kutaka kuwajaribu watu, kuwatakasa. Nyinyi nyote mnasema, “Mungu anawependaje wanadamu kwamba Anaweza kutayarisha miaka saba ya majaribu kuwatakasa watu na kuwafanya safi! Ni mvumilivu kiasi gani! Ni mwenye kuonyesha huruma kiasi gani!” Haina haja uyaseme haya, kila mmoja anaelewa mafundisho, lakini kwa hakika hakuna yeyote anayeifahamu hali halisi Je, miaka saba ya Mungu ya majaribu, miaka saba ya kazi ni ya nini? Bila shaka, inahitajika ili kwamba kazi Yake ifanyike. Hata bila kukuokoa, bado kuna upendo, sawa? Anapokuokoa, unasema, “Haya ni mapenzi aliyonayo Mungu kwetu, hii ni huruma Yake.” Je, Asingekuwa ametayarisha hii miaka saba ya majaribu, na kukamilisha kazi mara moja, bado kusingekuwepo upendo? Je, ingelikuwa miaka miwili ya majaribu, au mwaka mmoja, au siku ingalifika mara moja, je, hayo yasingekuwa mapenzi na huruma? Si kama unavyodhani: Miaka saba ya majaribu ni utakaso wa Mungu kwetu, ni kiwango Anachotupenda: ni lazima tutii. Unasema haya wakati tu hakuna njia nyingine. Hili linadhihirisha nini? Linadhihirisha uhasi, linadhihirisha lawama, na linadhihirisha kukosa njia mbadala na kukata tamaa. Mungu alisema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine. Wacha iwe miaka saba basi. Kisha unakurupuka na kusema maneno mazuri: Mungu, Unatupenda; Mungu, ni kwa ajili ya kututakasa. Bila miaka saba ya majaribu, je, huo usingelikuwa mwisho wetu? Kusingelikuwa na fursa. Watu wengine wanatamani kubarikiwa sasa hivi. Hiyo inaweza kuwa faida halisi! Mtu kama huyo hajali kitu kingine chochote kile. Mtu kama huyu hafai hata kwa senti moja. Kuna kazi ya vitendo katika hii miaka saba. Je, haijasemwa awali kwamba maneno mengine ni njia, lakini vilevile ni ukweli? Hakuna kipengele ambacho ni maneno tu bila matendo. Kila kipengele kina dhima. Aidha, kama aionavyo mwanadamu, takribani kila kipengele kina njia, lakini njia hii si ya kukurairai, si ya kukudanganya. Badala yake ni mazingira ya kweli, hali halisi Hakuna njia mwafaka kuliko hii. Baada ya kusikia maneno haya, watu wengine hufikiri: Ikiwa ni kama usemavyo, hii miaka saba inapoisha, ni nani anaweza kutambua umesalia muda kiasi gani! Kutokana na mijibizo ya watu inaonekana kuwa asili ya binadamu imewekwa kwa namna kwamba baada ya kukumbana na majaribu ya mateso, kupokea uchungu mwilini, anataka kuuepuka na kuukataa. Hakuna hata mtu mmoja hujitokeza na kuchukua hatua ya kudai: Mungu, nipe majaribu fulani ya kuteseka, nipatie dhiki fulani. Mungu, nipatie taabu zaidi. Hili linadhihirisha kuwa kiasilia watu hawapendi ukweli. Iwe ni kusudi la Mungu au la, au inafaidi watu vipi, haijalishi ni nzuri kiasi gani, watu wote hukataa hali yoyote inayoiletea miili yao machungu au ile isiyoafiki matamanio yao. Kuna watu wasemao: “Sipingi. Nilifanya uamuzi zamani kuyatoa maisha yangu yote kwa Mungu. Nina furaha kabisa haijalishi ni miaka mingapi, na nitamtumikia Mungu kwa moyo. Sina lawama. Haijalishi ninakumbana na majaribu gani, haijalishi ninakutana na mateso gani, iwe ni kutelekezwa na familia au maumivu ya ugonjwa, nitafuata hadi mwisho.” Huku kutokuwa na lawama kwako pia ni aina ya hali hasi, kwa sababu kila wakati unapokumbana na kitu chochote, kila wakati unaposemewa maneno, kwa hakika huelewi maana iliyo ndani. Hii “sina mjibizo” unayoisema kwa hivyo si kingine bali ni kutojali, njia wakati ambapo hakuna njia nyingine. Hakuna jingine la kufanya ila hili, kwa hivyo unajilazimisha kufuata hata wakati ambapo hauko radhi. Kwa vyovyote vile hakuna awezaye kufaulu kuepuka miaka saba ya majaribu. Hata hivyo, hii ni tofauti na wewe kutaka kutoroka. Ungetamani kuepuka lakini huwezi. Hili ni jambo la asili ya mwanadamu. Lifikirie. Je, ndivyo ilivyo? Watu wengine wanahisi: Nilipokumbana na tukio kama hili miaka kumi iliyopita, daima nilifuata, na niliteseka sana, kwa hivyo ninaweza kuendelea kuvumilia kwa miaka michache. Kutafuta kwenu kwa kusudi la Mungu kumekanganyikiwa na hamjakutilia maanani. Hivyo, ikiwa kwa ndani hujayatii mapenzi ya Mungu, basi umeyasaliti na kukana mapenzi ya Mungu. Ijapokuwa huna hali hii, na hujafanya jambo hili, hizi dalili, haya mambo yaliyo ndani yako, yanamkana Mungu, kwa sababu unachokifiria na kutarajia kwa ndani sicho Mungu anachokihitaji. Aidha kwa hakika humsifu Mungu kutoka ndani ya moyo wako kwa yote Anayohitaji kutoka kwako na yote Anayofanya, iwe ni njia, au kile ulichoambiwa.

Na kwa kila kitu Mungu ambacho anawataka watu wafanye, chochote Mungu alichowapangia watu kulingana na mahitaji yao, asili ya binadamu ni kukikataa, kukosa kukikubali. Haijalishi unautangaza vipi msimamo wako, au iwe una ufahamu kidogo, kwa vyovyote vile, ufahamu wako wa mafundisho hauwezi kutatua kilicho katika asili yako. Kwa hivyo ninasema kwamba watu wengi wanazungumzia vitu vizuri katika mafundisho, na kusema maneno ya juujuu kuyastahimili. Hatimaye, japo, katika maombi wanasema: Nimepitia kwa ufanisi miaka mingi sana. Miaka saba si miaka mingi na wala si miaka michache. Tazama ninavyozeeka, jinsi afya yangu ilivyoharibika, na kwamba sina familia nzuri. Nimeandamana na Wewe miaka hii yote, nifanya bidii hata bila malipo, nimechoka ijapokuwa sijafanya kazi kwa bidii. Hata kama Utaipunguza hata kwa miaka michache, nifanyie hisani mara hii moja! Unajua udahaifu wa watu… Kwa kuomba maneno haya, ni kama kuna utiifu kidogo. Wanaendelea kusema “Unajua udhaifu wa watu”; kuna maana nyingine ndani ya maneno haya, ambayo ni kusema, Unajua udhaifu wa binadamu, basi ni kwa nini inachukua muda mrefu kiasi hiki? Je, hii si hali iliyo ndani mwa watu? Kwa hivyo, mnahisi mnafahamu vitu vingi, tayari mmevikubali, na kuonekana mmefahamu ukweli, lakini kwa hakika bado mnaukataa ukweli, na kwenda kinyume cha ukweli. Vitu mnavyovifanya haviambatani na ukweli. Japo kijuujuu hamjafanya vitendo viovu, na hamjatamka kitu chochote kibaya, hii imejikita tu kwa kutovunja amri za utawala, kwa kutoikosea tabia ya Mungu. Hujaelewa kusudi Lake na hata hivyo hauko tayari kulipokea. Hukubaliani na Yeye kufanya mambo kwa njia hii. Unafikiri: Iwapo nitaifanya kazi hii, sitapoteza muda na nitaikamilisha kazi hii kwa muda mfupi iwezakanavyo, ili kwamba niwasaidie watu wa Mungu kuepuka mateso zaidi kutoka kwa joka kuu jekundu, kuzuia kupotea kwa watu wengi zaidi, kuepuka mateso yangu. Je, hili si wazo walilonalo watu? Watu mioyoni mwao wanatumaini kufika kwa ufalme wa Mungu, na kuangamia kwa haraka kwa ulimwengu wa Shetani. Ni neema kubwa ikiwa neno moja la Mungu litawabadilisha. Mitazamo ya ndani ya watu, matamanio yao makubwa kwa hakika hayatekelezi kusudi la Mungu, na kimsingi hakuna kiini cha kutii. Hili pia linagusa ule msemo: Asilimia mia moja ya kile kilicho ndani ya asili ya binadamu ni usaliti. Kwa hivyo, kwa kulichanganua hili au lile tukio lenu, kwa kulichanganua hili suala, lile wazo, au ile hisia, iwe unaikabili kwa njia hasi, au unalalamika, ikiwa hujali au umenyamaza bila kusema neno, kuna ukinzani katika haya yote. Haya yote ni usaliti. Je, huu uchanganuzi ni sahihi? Nisingalichanganua hili, kungekuwepo na watu wanaohisi: Ninaweza kudhaniwa kuwa mtu mzuri. Ningekumbana na jambo hili miaka michache iliyopita, bila shaka ningelalamika, ikiwezekana ningerudi nyuma, lakini sasa silalamiki. Hulalamiki, lakini je una uelewa? Je, uelewa wako mdogo unajumuisha uelewa wa kweli? Kuna ukweli ndani yake? Je, uelewa wako unalingana na kusudi la Mungu? Je, umepata kibali cha Mungu? Je, una kiini cha kumtii Mungu? Je, uko radhi na tayari kumtii Mungu? Kama sivyo, basi bila shaka unakinzana na Mungu. Inawezekana kwamba hali yako ya moyo sasa hivi ni nzuri, na hujihisi vibaya, au kwa sababu sasa hivi umewekwa katika kufanya kazi. Ikiwa siku moja utatumwa nyumbani, na utakapokuwa katika giza la hali mbaya ya moyo, hata hivyo, kilicho ndani ya moyo wako kitafichuliwa. Kuna watu wengine wenye kimo kidogo, wenye muda mfupi wa uzoefu ambao wanaweza kugeuka na kukimbia, kurudi ulimwenguni. Kwa hakika, katika uchanganuzi wa mwisho, mjibizo wowote ule ulionao, unakataa mazingira aliyokupangia Mungu. Asili ya watu ya kumsaliti Mungu inafichuliwa kila mahali. Ikiwa hili lisingechanganuliwa, watu wasingejijua kwa kina ipasavyo. Watu wakikumbana na kitu chochote, wote wanamsaliti Mungu na wanakosa kumtii. Mijibizo ya baadhi yenu ni kutotaka, au hisia za malalamiko, uhasi na huzuni, na mnasema: Kwa ndani, binadamu hapendi ukweli, na huku kutopenda si kingine bali ni usaliti. Bado haitoshi kama mnazungumza namna hii tu, na hamjachanganua hadi kwenye kina cha kiini. Mnasema kwamba kutopenda ukweli ni usaliti, lakini kwa kweli, hili si sahili hivyo Mmelichanganua vipi? Hamjielewi nyinyi wenyewe. Unaweza usijue hiyo ni hali gani uliyonayo, na huwezi kutofautisha mazuri na mabaya, ikiwa ni usaliti au la, na hujijui wazi wewe mwenyewe iwe umetii au la. Hamuwezi kuchanganua kabisa asili zenu wenyewe. Kila mara mnapokumbana na jambo fulani mnashindwa kujua namna ya kwenda mbele. Hatimaye, utakapokumbana na jaribu, je, utaweza kulitambua kusudi la Mungu? Utalifafanua hili vipi? Unapaswa kutembea katika njia gani? Ni mantiki gani au ni ukweli gani unapaswa kuwa nao ili kukidhi kusudi la Mungu? Kama kiwango cha chini zaidi, ni lazima uwe na mtazamo chanya. Je, mmeyawazia maswali haya?

Zamani watu wengine walikuwa na mawazo kuhusu anachokifanya Mungu mwenye mwili. Ushirika uliofuata ulisababisha kuwepo na ukweli usiohitaji uthibitisho. Ukweli huu usiohitaji uthibitisho ni: Binadamu wanapaswa kukiri kuwa yote anayofanya Mungu ni sahihi, kuwa yote ni muhimu. Kama binadamu hawataelewa wanapaswa hata hivyo kutii na si kupinga. Kama binadamu wana mawazo ni lazima wataaibika. Je, watu wanakumbuka maneno haya? Kila mara wanapokabiliana na kitu, wanajisemea wao wenyewe: Kwa namna yoyote usiwe na mawazo, kwa namna yoyote usiyahukumu. Kuna maana katika kila kitu anachokifanya Mungu. Ijapokuwa hatuwezi kuelewa kwa sasa, siku moja tutapata aibu. Wanazishikilia tu sheria kama hii. Sheria ya aina hii, hata hivyo, yaweza kusuluhisha matatizo kadhaa ya waumini ambao wamekanganyikiwa. Kwa mtu aliye na uelewa haya maneno yatasaidia kuelewa maana ya vitu vingi, na kutumia hii sheria kila mara hali inaposhuhudiwa yaweza kuweka wazi mambo mengi. Ni nini kinachofanyika kama hakuna umaizi? Mtu anaweza tu kutii sheria, na katika kufanya hivyo anaweza pia kulindwa na kuzuia kukiuka amri za utawala, si kueneza maafa. Sheria hii ina manufaa! Sio ati haina maana! Katika sehemu mbalimbali sheria hii imesomwa kwa moyo. Wengine huiandika madaftarini, au kuiandika kwenye jalada la kitabu, na kuisoma kila wakati wanapofungua kitabu, huku wakiikariri. Wanaikariri wanapoomba. Kufanya hivyo kuna manufaa kadhaa. Watu wengine hawathubutu kufanya mambo kwa kubahatisha, na wana uchaji mdogo mioyoni mwao. Ila kulingana na watu wengi, hawana uelewa wa kweli wa hali chanya, na kuna vitu vingi sana vilivyo hasi. Ijapokuwa inaonekana kuwa mnajihisi vyema kabisa na hamjaacha kufanya kazi, kuna vitu vingi hasi kwa kweli kati yenu, na hakuna vitu chanya. Kuna mijibizo mingi sana kanisani kuhusu mambo kama haya. Je, mmejaribu kujijumuishia nyinyi wenyewe? Kama vitu vya aina hii vingekabiliwa tena, mngemkataa Mungu au kumsaliti Mungu? Kuna baadhi ya watu ambao labda wametambua, "Binadamu hana uwezo wa kuielewa asili yake mwenyewe. Bila shaka sitajaribu kukataa tena, na lazima niwe makini. Lazima niombe kila siku!” Huu sio mpango wa uhakika. Nimegundua kuwa huwa mnapata aibu, na mara nyingi mnasema: "Ah, nitafanya nini kuhusu hii asili ya binadamu? Siwezi kuisuluhisha mimi mwenyewe, na siwezi kuielewa. Kwa kweli sina haki ya kujisimamia mimi mwenyewe. Sijui ninaweza kufanya nini siku moja. Ninaogopa sana. Kumwamini Mungu lazima kufanyike kwa makini mno. Uzembe wowote waweza kusababisha maafa, na hilo laweza kuwa jambo baya mno. Hata sijijui, siwezi kujitegemea..." Ingawa watu wanaosema haya mara kwa mara huwa wanajielewa kwa kiasi fulani, wana uelewa kidogo mno kuhusu ukweli. Wanachanganyikiwa kila mara wanapokumbana na kitu chochote. Wanapatwa na wasiwasi, wanahisi uoga, na hawana njia yoyote ile wanapopatwa na chochote kile. Wakati huu umeshinda miaka saba ya majaribu, na hujasababisha maafa, na hujakiuka amri za utawala, lakini je, waweza kuwa na uhakika kuhusu wakati ujao? Wawezaje kuyashinda haya yote bila kizuizi? Unaona kuwa umeyashinda masaibu kwa urahisi sana, kwa kujificha hapa na pale. Ulijificha kwa mwaka mmoja au nusu mwaka hadi yakaisha. Wanadamu wanaweza kujificha, lakini asili ya binadamu ni kitu ambacho hakiwezi kufichika. Je, hakupaswi kuwa na ukweli uisohitaji thibitisho unaohusiana na hili, pia? Katika kila majaribu ya Mungu kuna nia nzuri. Kwa kila tukio linaloshuhudiwa kuna ukweli ambao mtu anapaswa kuwa nao ili kusimama imara. Jiandaeni na ukweli ili kukabiliana na majaribu tofauti tofauti kwa sasa, na hamtaogopa bila kujali miaka ya majaribu hapo mbeleni. Lazima muwe na ujasiri. Kutii mipango ya Mungu kamwe hakuwezi kuwa na dosari. Njia daima itakuwa na matumaini. Mwawezaje kuwa wakamilifu bila majaribu kadhaa? Bila majaribu, hakuna shahidi. Ni vipi basi mtamridhisha Mungu? Majaribu yatawaletea baraka za Mungu. Ni kwa kumfuata tu Mungu hadi mwisho ndipo mtu aweza kuingia katika ufalme. Kumbuka: nyinyi nyote mna fungu katika dhiki, ufalme, na uvumilivu wa Kristo.


kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Ijumaa, 1 Februari 2019

Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days

Filamu za Injili | "Nimewahi Treni ya Mwisho" | Entering the Ark of the Last Days

Chen Peng alikuwa mchungaji katika kanisa la nyumba fulani. Alikuwa akimtumikia Bwana kwa bidii, na mara nyingi alifanya kazi kama mhubiri, akiwasaidia wafuasi wake, na kulibebea kanisa mizigo mizito. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kanisa lilizidi kuwa tupu zaidi na zaidi. Waumini walikuwa na roho dhaifu na wavivu, wakikosa mkutano baada ya mkutano. Na hivyo Mchungaji Chen aliona giza likiangukia nafsi yake, kana kwamba kisima cha roho yake kilikuwa kikavu, na hakuweza kuhisi uwepo wa Bwana. Katika mikutano, aligundua kwamba hakuwa na kitu alichoweza kuhubiri. ... Alifanya kila kitu alichoweza kufikiria ili kuimarisha kanisa, lakini jitihada zake zote zilikuwa bure. ... Chen Peng alikuwa amesitikika, amepotea, na hakuweza kuelewa kwa nini kanisa lake lilikuwa linajawa na ukiwa sana, na kwa nini walikuwa wamepoteza uwepo wa Bwana.
Hadi siku moja, kwa bahati, aliposikia injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Baada ya kupitia mjadala mkali, Chen Peng hatimaye aligundua sababu ya kanisa lake kuwa na ukiwa, na akaamini kwamba Mungu alikuwa tayari amekuwa mwili na kuwa Mwana wa Adamu: Mwenyezi Mungu, anayehukumiwa na kutelekezawa na ulimwengu wa kidini, ambaye anasema ukweli na kufanya kazi ya hukumu katika zile siku za mwisho! Ni wale tu ambao wanakubali kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa zile siku za mwisho, na kufuata nyayo za Mwana-Kondoo wataweza kunyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kufikia kunyunyuziwa na kupewa maji ya uzima. Kwa sababu ya hilo, Chen Peng aliwahi treni ya mwisho na kukubali kwa furaha kazi ya Mungu katika zile siku za mwisho.

Alhamisi, 31 Januari 2019

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?

Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP. Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa. Wakati huu, meya anapokea taarifa za kipaumbele kutoka Kamati Kuu ya Chama, baada ya hapo anajaribu kutafuta njia za kumlazimisha Liu Ming'en na mkewe kuweka saini barua ya kuahidi kuacha kuamini katika Mungu. Baada ya hila yake kushindwa, polisi tena wanakuja kuwakamata waumini hawa wawili. Kuepuka kukamatwa na kuendelea kumfuata Mungu na kuamini katika Mungu, Liu Ming'en na mkewe wanalazimishwa kutoroka nyumbani kwao.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumatano, 30 Januari 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa au mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, haya si makosa kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umetosha kuwafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Hii ni kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka au wataanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu hasa katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si mkubwa tu, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini. Na kwa hivyo, watu humtendea kama mtu wa kawaida; wao hufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja naye, na kusema maneno kiholela Kwake, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa "Kristo wa kweli." Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza kabisa.”

Jumanne, 29 Januari 2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Uendelezo wa Sehemu ya Pili

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)” Uendelezo wa Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Tofauti na Pana Yaonyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu Hakuna Kiumbe Chochote Kati ya Vile Vilivyoumbwa na Vile Ambavyo Havikuumbwa Kinaweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Jumatatu, 28 Januari 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Pili

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Pili

Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Pili Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza 1. Maisha Mapya Yanazaliwa Kulingana na Mipango ya Muumba 2. Kwa Nini Binadamu Tofauti Wanazaliwa Katika Hali Tofauti Kukua: Awamu ya Pili 1. Hali Ambazo Mtu Hukulia Ndani Zimepangwa na Muumba 2. Hali Mbalimbali Ambazo Watu Hukulia Ndani Husababisha Wajibu Tofauti
Mwenyezi Mungu alisema, Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Unachukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu wa Mungu. Unaanza safari ya maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeweka, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake, kwa maana Anayetawala juu ya kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa thabiti katika kazi Yake, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na harakati ya mambo yote. Kama kila kiumbe, mwanadamu bila kujua anapata lishe ya utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatunzwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, vilivyo hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hivi ndivyo Mungu anavyotawala juu ya kila kitu.
kutoka kwa Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Jumapili, 27 Januari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”

Mwenyezi Mungu anasema, “‘Kumwogopa Mungu na kuepuka maovu’ na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri. Iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kuepuka maovu, lazima kwanza amche Mungu kwa kweli; iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kumcha Mungu kwa kweli, lazima awe na maarifa ya kweli kuhusu Mungu; Iwapo mtu anataka kupata maarifa ya Mungu, lazima kwanza ayapitie maneno ya Mungu, aingie katika ukweli wa maneno ya Mungu, apitie kuadibu na nidhamu ya Mungu, kuadibu Kwake na hukumu; iwapo mtu anataka kupitia maneno ya Mungu, lazima aje ana kwa ana na maneno ya Mungu, aje ana kwa ana na Mungu, na kumwomba Mungu Ampe fursa ya kupitia maneno ya Mungu katika hali ya aina yote ya mazingira inayowahusisha watu, matukio na vitu; iwapo mtu anataka kuja ana kwa ana na Mungu na maneno ya Mungu, lazima kwanza amiliki moyo wa kweli na mwaminifu, awe tayari kuukubali ukweli, kukubali kupitia mateso, uamuzi na ujasiri wa kuepuka uovu, na azimio la kuwa kiumbe halisi…Kwa njia hii, kuendelea mbele hatua kwa hatua, utamkaribia Mungu zaidi, moyo wako utakuwa safi zaidi, na maisha yako na thamani ya kuwa hai, pamoja na maarifa yako kumhusu Mungu, yatakuwa ya maana zaidi na yatakuwa hata ya kupevuka zaidi.”

Jumamosi, 26 Januari 2019

Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 56. Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

Upendo wa Mungu, ambaye alikuwa mwili, unajidhihirisha wapi kwa binadamu? Baada ya kupitia uzoefu wa kazi hatua kwa hatua, mnaweza kuona kwamba Mungu anapozungumza katika kila hatua ya kazi, anatumia ruwaza fulani, anazungumza unabii fulani, na anaonyesha ukweli fulani na tabia ya Mungu, na watu wote wana mijibizo. Mijibizo yao ni nini? Hawajinyenyekeshi kwa Mungu, hususan hawachukui hatua ya kutafuta ukweli, au hawapo radhi kukubali kazi ya Mungu. Wote wana mitazamo hasi na wabishi, na wanakanganyikiwa, wanakataa na hawakubali. Hata hivyo, toka mwanzo, Mungu hajabadilisha namna Anavyofanya kazi Yake, upendo Wake kwa binadamu haubadiliki. Bila kujali mtazamo wa watu, bila kujali kama wanakataa au wanakubali shingo upande, au wanabadilika kidogo, upendo wa Mungu haubadiliki. Kazi Yake haijawahi kuvurugwa katika hatua yoyote ile. Hiki ni kipengele kimojawapo ambapo upendo Wake unadhihirishwa. Aidha, baada ya kila hatua ya kazi kukamilika, bila kujali namna ambavyo watu wanajidhihirisha, upendo wa Mungu kwa watu haubadiliki. Siku zote Anafanya kazi na siku zote Anawaokoa watu. Katika hatua inayofuata Anapokuwa anafanya kazi Yake, maneno Yake ya hukumu na ufunuo yatakuwa ya kina, wazi zaidi, na kuelekezwa zaidi katika hali ya sasa ya watu. Anazungumza maneno fulani kuwaruhusu watu waweze kumuelewa na kumfahamu Yeye vizuri zaidi, na hususan ili kwamba waweze kuelewa mapenzi Yake na waweze kupata mapenzi Yake. Watu wataona kwamba Mungu bado Anawapenda binadamu. Bila kujali kama mijibizo ya watu siku zote kuwa ni hasi au inampinga Mungu, watu siku zote watakuwa na aina hii ya mijibizo katika kila hatua ya kazi. Hata hivyo, Mungu siku zote huzungumza na hufanya kazi, na Mungu kamwe hajawahi kubadili upendo Wake kwa binadamu. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu kwa binadamu ni upendo. Baadhi ya watu husema: "Kama yote ni upendo, basi kwa nini Anahukumu na kumwadibu mwanadamu? Kwa nini inaonekana ni chuki kwa watu? Hata anawajaribu watu na kuwaacha wafe!" Ni kweli, Mungu ana upendo tu kwa watu! Mungu huurudi na kuuhukumu uasi wa watu ili kuwafanya watu waelewe ukweli na kuwafanya watubu na kuanza upya, na kuwafanywa watu waielewe tabia ya Mungu, na hivyo kuwafanya watu kumheshimu Mungu na kujinyenyekesha Kwake. Baadhi ya watu akili zao zipo katika hali ya kupinga, lakini Mungu hakati tamaa hata kidogo katika kuwaokoa watu; hii huhitaji kiwango kikubwa cha upendo, sio? Wakati wa kipindi cha wafanya huduma, watu wengi wapo katika hali ya uhasi na maumivu kiasi kwamba wanalia na kuhangaika kwa kiasi ambacho wanaomboleza na kulalama kwa sauti, wakijiuliza wanawezaje kuwa wafanya huduma katika shida nyingi kiasi hicho. Kwa kweli hawako radhi! Hauko radhi na huelewi, lakini Mungu anakuelewa. Je, huu si upendo? Upendo Wake unajumuisha ufahamu wa watu, kuwaongoza watu wote, na uelewa wa kina wa watu. Upendo Wake haukanganywi, si wa kujifanya, si mtupu, bali ni wa kweli. Anauona upungufu na ujinga wako na Ana huruma juu yako, Anakupenda na siku zote Anakuamsha kihisia. Bila kujali kama upo tayari au haupo radhi kuwa mfanya huduma, siku zote Anazungumza na kukupatia miezi kadhaa ya utakasaji ili kufunua ufisadi wako na kukufanya uifahamu hali yako ya fedheha. Je, kunakuwa na upendo wakati wa kipindi hiki cha miezi mitatu? Kama Hakuwa na upendo, basi Angekupuuza; kwa kutazama mwenendo wako wa mambo wakati wa kipindi cha wanfanya huduma, Angekuwa amekusukumilia mbali mapema. Je, hauko radhi kuwa mfanya huduma? Hutoteswa na Mungu, lakini unarukaruka kwa furaha pale unapopata baraka. Ikiwa Mungu alikuwa na chuki pekee badala ya upendo, basi watu wangeangamizwa kwa sababu ya mijibizo yao miovu. Miezi mitatu ya utakasaji si muda mrefu. Kwa nini Nasema sio muda mrefu? Kwa sababu hiki ni kiasi tu cha muda ambao watu wanaweza kuvumilia. Kama ingekuwa kwa muda mrefu kidogo, basi wasingeweza kuvumilia. Ingawa siku zote wanaimba, wanakutana pamoja, na kushiriki, wanafurahia tu mambo hayo na hakika wasingeweza kuendelea kusimama; kwa hiyo, wanabadilishwa kuwa watu wa Mungu mapema Hii pia inahitaji upendo; Mungu anatumia moyo Wake na upendo kuwabadilisha watu na kuwashikilia watu. Huu pia ni udhihirishaji wa upendo. Unaweza kuona upendo wa Mungu katika kipindi cha muda huu; hachelewi hata kwa siku moja au mwezi mmoja. Siku itakapofika ambapo Atapaswa kuzungumza, basi huzungumza bila kuchelewa. Kama Angechelewa miezi mingine michache, basi hatua kwa hatua baadhi ya watu wangeondoka. Huku ni kufanya kazi kulingana na hali halisi za watu. Hachelewi kabisa au kupoteza muda, Anamzingatia kila mtu kwa umahususi. Kwa kuwa Anawaokoa watu, Anawajibika hadi mwisho. Lakini baadhi ya watu hawayaishi matarajio, wanateleza na kuanguka chini. Kabla ya watu hawajaondoka, Roho Mtakatifu kwa umahususi anawasukuma na kuwasihi wabaki. Baadhi ya watu kwa kweli wamebembelezwa kubaki lakini hawakubaki. Mungu kwa kweli anawapenda watu sana, lakini watu hawamruhusu Mungu kuwapenda. Ikiwa Mungu hawezi kuwapenda watu wanaojiondoa, basi itabadilika kuwa chuki, na Anaweza kumpuuza kabisa mtu wa aina hiyo. Kwa kuzingatia hatua na kiwango cha muda wa kazi, urefu wa hatua, kiasi cha maneno yaliyosemwa katika hatua, toni ya sauti, mbinu zilizotumika katika hatua, na ukweli unaoambatana nayo kukufanya uelewe, yote hujumuisha mawazo Yake makuu na tafakari na mpangilio na upangaji sahihi. Siku zote Anatumia hekima Yake kuwaongoza binadamu, kuwakimu, kuwahudumia, na kuwakuza kidogokidogo na kuwaleta katika siku hii. Kila mtu ambaye amepitia mambo haya sasa ana kiasi fulani cha ufahamu; hata kama Siijadili, watu wengi wanaweza; watu wanaweka mchakato wa hatua kwa hatua katika kumbukumbu zao. Hakuna maneno ya kuelezea upendo uliopo katika hili. Mungu anawapenda watu sana lakini watu hawataupitia upendo huo kwa kina; upendo huu ni wa kina sana na haiwezekani kuuelezea vizuri kwa maneno; haiwezekani kuuelezea kwa mtazamao wa wakati. Kwa mtazamo wa wakati, tunaweza kuona ni jinsi gani upendo Wake kwa binadamu ni wa kina sana; Anatoa uangalifu mkubwa kwa mambo madogomadogo na haruhusu muda kusonga hata kidogo. Anahofia kwamba ikiwa muda utasonga sana watu watajiondoa na kumwacha. Upendo Wake unawashikilia watu kwa nguvu na haukati tamaa kabisa. Aidha, kuna hatua za kurudi na hukumu pia ambazo Mungu Anazifahamu. Ikiwa kungekuwa na mbinu nyingine zaidi, watu wangehisi kwamba Mungu alikuwa Anawahadaa na kuwachezea. Vimo vya watu havijafikia kiwango na ni rahisi sana kwao kujitoa. Kwa hiyo, baada ya miezi mitatu ya utakasaji, Mungu alizungumza tena na kuwafanya wafanya huduma kuwa watu Wake na kila mtu alifurahi. Watu walitikiswa kihisia kiasi kwamba wakaangua kilio na wakaona kwamba hekima ya Mungu ni nzuri sana. "Wakati huo wote nilidhani nilikuwa mfanya huduma kweli, nilidhani sina hatima, na kwamba hii ilimaanisha kwamba Mungu hatutaki na tumekwisha kabisa." Wakati huo kama Ningesema kwamba nisingewaruhusu kufa, hakuna ambaye angeamini; mngedhani kwamba Mungu tayari amesema hivyo na kwamba ilikuwa ni kweli kabisa. Baada ya miezi mitatu, Nilizungumza kifungu kingine cha maneno na kuhitimisha hukumu ya wafanya huduma. Ingawa asili za watu zimepotoka, wakati mwingine watu wanakuwa hawana hatia hasa kama mtoto mdogo. Kwa nini inasemwa kwamba watu siku zote ni watoto wachanga mbele ya Mungu? Kila tendo wanalofanya ni kama la mtoto mchanga; watu wanawaangalia wengine kana kwamba wote wamepotoka na kuoza, lakini katika macho ya Mungu, watu siku zote ni watoto wachanga, wanyofu na wasio na hatia; kwa hiyo Mungu hawachukulii watu kama maadui, badala yake Anawaangalia kama walengwa Wake wa wokovu na upendo. Kwa hiyo upendo wa Mungu kwa watu si kama ambavyo watu wanafikiria, ambayo ni kusema tu mambo mazuri na heri. Wakati huu, kuna maneno fulani katika kazi ya Mungu ambayo kwa kweli hayakidhi matarajio ya watu, hadi kufikia hatua ya kuvunja mioyo ya watu na kuwasababishia maumivu. Baadhi ya maneno ya hukumu ni kama yanawachora na kuwakaripia watu, lakini kwa kweli yote yana muktadha wa kweli na yapo sambamba na uhakika na ukweli. Hayajaongezwa chumvi. Mungu anazungumza kulingana na dutu ya watu iliyopotoka na kwa kuwa watu watapitia uzoefu kwa kipindi fulani, basi wataelewa. Kusudi la Mungu kusema mambo haya ni kuwabadilisha na kuwaokoa watu. Ni kwa kuzungumza tu kwa namna hii ndiyo Anaweza kupata matokeo mazuri kabisa. Unapaswa kuona kwamba nia njema ya Mungu ni kwa ajili ya kuwaokoa watu na kila kitu kilichomo ndani yake ni upendo wa Mungu. Bila kujali kama unauangalia kwa mtazamo wa hekima katika kazi ya Mungu, kwa mtazamo wa hatua na ruwaza katika kazi ya Mungu, au kwa mtazamo wa wakaa wa kazi au mipangilio na mipango Yake sahihi—chote kilichomo ndani yake ni upendo Wake. Kwa mfano, watu wote wana upendo kwa wana na mabinti zao na ili kuwaruhusu watoto wao kutembea katika njia sahihi, wote wanaweka jitihada kubwa. Wanapogundua udhaifu wa watoto wao, wanahofia kwamba ikiwa watazungumza kwa sauti laini, watoto wao hawatasikia na hawataweza kubadilika, na wanahofia kwamba ikiwa watazungumza kwa ukali sana, wataumiza staha ya watoto wao na watoto wao hawataweza kuvumilia. Kwa hiyo, hii yote inafanyika chini ya ushawishi wa upendo na kiwango kikubwa cha jitihada kinatumika. Nyinyi ambao ni wana na mabinti mtakuwa mmeshawahi kupata upendo wa wazazi wenu. Sio tu upole na kujali ndio upendo, lakini hata zaidi, kuadibu sana ni upendo. Mungu yupo chini ya ushawishi wa upendo kwa binadamu na chini ya sharti la mwanzo la upendo. Kwa hiyo, Anafanya kwa kadri ya uwezo Wake wote kuwaokoa wanadamu waliopotoka. Hashughuliki nao kwa kutimiza wajibu tu, badala yake anafanya mipango sahihi, kulingana na hatua. Kwa kuzingatia wakati, eneo, toni ya sauti, mbinu ya kuzungumza, na kiwango cha jitihada kilichowekwa..., mnaweza kusema kwamba yote hii inafunua upendo Wake, na inaelezea vizuri kabisa kwamba upendo Wake kwa binadamu hauna mipaka na haupimiki. Na watu wengi wanasema maneno ya uasi wanapokuwa katikati ya kujaribiwa kwa mfanya huduma na wanatoa malalamiko. Lakini Mungu hagombanigombani juu ya mambo haya, na hakika hawaadhibu watu kwa hili. Kwa sababu Anawapenda watu, Anasamehe kila kitu. Ikiwa Angekuwa na chuki tu badala ya upendo, basi Angeweza kuwahukumu watu mapema kabisa. Kwa kuwa Mungu ana upendo, Hagombanigombani, bali Anavumilia, na Anaweza kuona shida za watu. Hii kabisa ni kufanya kila kitu chini ya ushawishi wa upendo. Mungu tu ndiye anawaelewa watu, wewe hata hujielewi. Hiyo si sahihi? Tafakari kuhusu hilo kwa makini, baadhi ya watu wanalalamika kuhusu hiki na kile; watu wanasababisha shida bila sababu, wanaishi kwenye baraka lakini hawahisi baraka. Hakuna Anayejua ni maumivu kiasi gani Mungu ambaye Alishuka duniani kutoka mbinguni atalazimika kuteseka kiasi gani. Mungu alikuwa mtu, Yeye ni mkuu sana na Aliweza kuwa mdogo hivyo, wa hali ya chini na Aliteswa hivyo. Ni maumivu kiasi gani Aliyopitia! Chukua mfano kutoka duniani: Mtawala mzuri huwapenda watu wake kama tu watoto wake, na ili kuelewa shida na mateso ya watu, yeye binafsi anatoka na kwenda kushuhudia. Kulinagana na nafasi yake, hapaswi kuteseka na maumivu haya, lakini ili kuondoa maumivu ya watu, anawatembelea kwa siri akiwa katika mavazi ya kawaida. Anakwenda miongoni mwa watu na kushuhudia na kuyaelewa maumivu ya watu kama mtu wa kawaida. Kulingana na nafasi yake, kujishusha hadhi kwenye hadhi ya mtu wa kawaida ni jambo la unyenyekevu; anapaswa kuishi kama mtu wa kawaida na watu hawaijui hadhi yake, na kwa kweli wanamchukulia kama mtu wa kawaida. Kuna hatari nyingi miongoni mwa watu, na kimsingi wanamchukulia kwa namna tofauti, na huanza kupata shida na mateso ya watu; huteseka kwa maumivu ambayo watu wanawayapata; analazimika kuwa mwangalifu na makini kila mahali. Anafanya hivi kwa ajili gani? Kuna lengo moja tu linalomsukuma. Mungu anaweza kufanya kazi kwa namna hii leo kwa sababu mpango Wake wa usimamizi umefikia kiwango hiki. Anawapenda binadamu hivyo Anawaokoa binadamu, Anaweza kufanya hili kwa sababu Anasukumwa na upendo na yupo ndani ya viunga vya upendo. Mungu alikuwa mwili na Aliteseka kwa mateso makubwa ili kuliokoa kundi hili la binadamu walioharibika. Hii kwa kutosheleza kabisa inathibitisha kwamba upendo Wake ni mkubwa sana. Kuna ushauri, faraja, tumaini, uvumilivu, na ustahimilivu katika maneno ambayo Mungu huzungumza, hata zaidi, kuna hukumu, adibu, laana, kufichuliwa hadharani, ahadi za kuvutia, n.k. katika maneno Yake. Bila kujali mbinu, yote hii imetawaliwa na upendo. Hii ni dutu ya kazi Yake, sio? Nyinyi nyote kwa sasa mna kiasi fulani cha uelewa, lakini sio wa kina kiasi hicho. Angalau mnaweza kuwa na kiasi fulani cha ufahamu, na baada ya kuwa na uzoefu wa miaka mitatu hadi mitano, mtaweza kuhisi kwamba upendo huu ni wa kina sana na ni mkubwa sana. Haiwezekani kutumia meneno ya binadamu kuelezea. Ikiwa watu hawana upendo, wanawezaje kurudisha upendo wa Mungu? Hata kama uliyatoa maisha yako kwa Mungu, usingeweza kumlipa. Baada ya nyinyi kupitia uzoefu wa mika mitatu hadi mitano, na kutafakari juu ya mafunuo na tabia zenu za sasa, mtakuwa na majuto kupita kiasi na mtapiga magoti chini na kusujudu vichwa vyenu kwenye ardhi. Kwa nini watu wengi wanafuatilia kwa karibu? Kwa nini watu wengi wamekuwa na shauku kubwa hivi? Wana uelewa wa upendo wa Mungu, na wanaona kwamba kazi ya Mungu ni kuwaokoa watu. Fikiria kuhusu hilo, je, kazi ya Mungu sio sahihi hususan kwa kuzingatia muda? Kiungo kimoja hufuata kiungo kingine bila kuchelewa hata kidogo. Kwa nini Hachelewi? Bado ni kwa ajili ya binadamu. Hayupo radhi kutoa sadaka au kupoteza roho hata moja. Watu hawajali kuhusu majaliwa yao wenyewe, kwa hiyo, ni nani katika dunia hii anakupenda sana? Hujipendi, hujui kutunza maisha yako mwenyewe, na hujui yana thamani kiasi gani. Ni Mungu Ndiye Anayewapenda sana binadamu. Ni Mungu pekee ndiye Anayewapenda sana binadamu. Watu wanaweza kuwa bado hawajaliona hili, wakidhani kwamba wanajipenda. Kwa kweli, ni upendo gani ambao watu wanao wao kwa wao? Ni upendo wa Mungu tu ndio upendo wa kweli; taratibu utaelewa upendo wa kweli ukoje. Ikiwa Mungu hangekuwa mwili na kufanya kazi na kuwaongoza watu uso kwa uso, ikiwa Hangekutana na watu na kuishi na watu wakati wote, basi kuuelewa upendo wa Mungu kwa kweli kisingekuwa kitu rahisi kwa watu kufanya.

Watu na Mungu kimsingi hawafanani na wanaishi katika dola mbili tofauti. Watu hawawezi kuielewa lugha ya Mungu, na zaidi hawawezi kuyaelewa mawazo ya Mungu. Ni Mungu pekee ndiye Anayewaelewa watu na haiwezekani kwa watu kumwelewa Mungu. Mungu ni lazima Awe mwili na Afanane na mwanadamu (kufanana kwa umbo la nje). Mungu anavumilia mateso na maumivu mengi ili kuwaokoa binadamu na kuwafanya watu kuielewa na kuifahamu kazi ya Mungu. Kwa nini Mungu siku zote Anawaokoa watu na hajawahi kukata tamaa? Hii si kwa sababu ya upendo Wake kwa watu? Anamwona binadamu akiharibiwa na Shetani na Hawezi kuvumilia kuacha au kukata tamaa. Kwa hivyo kuna mpango wa usimamizi. Ikiwa Angewaharibu binadamu Akipatwa na hasira kama watu walivyodhani, basi kusingekuwa na haja ya kuwaokoa watu waziwazi kwa namna Afanyavyo sasa. Na kwa kuwa Alikuwa mwili na Akateseka kwa maumivu, upendo Wake umedhihirishwa, upendo Wake unavumbuliwa kidogokidogo na watu na unafahamika kwa watu wote. Kama isingekuwa kwa kufanya kazi namna hii sasa, na ikiwa watu wangejua tu kwamba kuna Mungu mbinguni na kwamba Anawapenda binadamu, basi hili litakuwa ni fundisho tu, na watu kamwe wasingeweza kuuona upendo wa Mungu. Ni kwa Mungu tu kuwa mwili na kufanya kazi ndipo watu wanaweza kuwa na uelewa wa kweli juu Yake ambao si wa kufikirika au mtupu na wala sio maneno matupu, lakini badala yake ni ufahamu ambao ni wa kweli. Hii ni kwa sababu upendo ambao Mungu anawapatia watu ni wa manufaa yanayoonekana, kazi hii inaweza kufanywa tu kwa kuwa mwili na haiwezi kuchukuliwa nafasi na Roho Mtakatifu. Ni upendo mkubwa kiasi gani ambao Yesu aliwapa watu? Alihudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu waliopotoka kwa kusulubiwa, Alikuja kukamilisha kazi ya ukombozi kwa ajili ya binadamu, hadi aliposulubiwa. Upendo huu hauna mipaka na kazi ambayo Mungu ameifanya ni ya muhimu sana. Kuna watu ambao wana dhana kuhusu Mungu kuwa mwili. Ni dhana gani hizi walizonazo? Bila Mungu kuwa mwili, imani ya watu kwa Mungu ingekuwa ni mfumo tupu na wakati wa mwisho wangeangamizwa. Upendo wa Mungu kwa binadamu hasa umedhihirishwa katika kazi Yake wakati akiwa katika mwili, Yeye binafsi Akiwaokoa watu, Akizungumza uso kwa uso na watu, na kuishi miongoni mwa watu bila kuwa mbali nao hata kwa hatua moja, bila kujifanya, lakini akifanya kweli. Huwaokoa watu kwa kiasi kwamba Aliweza kuwa mwili na kupita miaka mingi ya maumivu pamoja na watu duniani, yote hii ni kwa sababu ya upendo Wake na huruma kwa binadamu. Upendo wa Mungu kwa binadamu hauna masharti au matakwa. Anapata nini kutoka kwa binadamu? Watu hawamchangamkii Mungu. Nani anaweza kumchukulia Mungu kama Mungu? Watu hata hawampatii Mungu faraja, hata leo hii Mungu hajapokea upendo wa kweli kutoka kwa watu. Mungu Anatoa bila ubinafsi na Anakimu bila ubinafsi, lakini watu bado hawaridhiki na wanaendelea kuomba neema bila kukoma. Watu ni wagumu sana kushughulika nao na ni wasumbufu sana! Hata hivyo, siku moja siku itafika ambapo kazi ya Mungu itapata matokeo na idadi kubwa ya watu watatoa shukrani za kweli kutoka mioyoni mwao. Watu ambao wamepitia uzoefu wa miaka mingi wanaweza kuelewa kipengele hiki. Ingawa watu ni wazito, hata hivyo sio maroboti; si vitu visivyokuwa na uhai. Watu ambao hawajawahi kuwa na uzoefu na kazi ya Mungu wanaweza wasieweze kutambua mambo haya; wanakubali kwa kusema kwamba ukweli huu ni sahihi, lakini hawana uelewa wa kina sana.

Mungu alikuwa mwili na Amefanya kazi kwa miaka kadhaa na Amesema mambo yasiyoweza kuhesabika. Mungu anaanza kwa kutoa hukumu ya wafanya huduma, na baadaye Husema unabii na Huanza kazi ya hukumu na kurudi, kisha Hutumia kifo kuwatakasa watu. Baada ya hapo, Huwaongoza watu katika njia sahihi ya kumwamini Mungu, Akizungumza na kuwapatia watu ukweli wote na kupambana na dhana mbalimbali za mwanadamu. Baadaye, Humpatia mwandamu tumaini dogo kumruhusu kuona kuna tumaini mbele yake; yaani, Mungu na watu wanaingia katika mwisho mzuri wa safari kwa pamoja. Ingawa kazi hii inafanywa kulingana na mipango ya Mungu, yote inafanywa kulingana na mahitaji ya binadamu. Haifanywi kiholela na Yeye; Hutumia hekima Yake kufanya kazi yote hii. Kwa kuwa ana upendo, Anaweza kutumia hekima na kwa bidii kushughulika na watu hawa walioharibika. Hachezi na watu hata kidogo. Hebu angalia toni ya sauti na namna ya kutamka maneno katika maneno ya Mungu; wakati fulani inawapatia watu majaribu, wakati fulani meneno Yake huwafanya watu kutahayari, wakati fulani huwapatia watu maneno ambayo huwaokoa na hufanya wawe watulivu. Kwa kweli Anawafikiria sana na kuwajali watu. Ingawa watu ni viumbe wa Mungu, na wote wamepata uharibifu kutoka kwa Shetani, na ingawa watu hawana thamani, ni wazururaji, na asili zao ziko namna hii, Hashughuliki na watu kulingana na hulka zao, na Hashughuliki nao kulingana na adhabu ambayo wangestahili kuipata. Ingawa maneno Yake ni makali, siku zote Anashughulika na watu kwa ustahimilivu, uvumilivu, na huruma. Tafakari hili kwa taratibu na kwa makini! Ikiwa Mungu hakushughulika na watu kwa uvumilivu, huruma na neema, je, Angeweza kusema mambo haya yote ili kuwaokoa watu? Kwa nini Hakuwahukumu watu moja kwa moja? Watu ni wapumbavu sana na wajinga, watu hawana upendo katika dutu yao, na hawajui upendo ni nini, na hawajui kwa nini Mungu hufanya kazi namna hii. Watu wanapokuwa hawauoni upendo wa Mungu, basi wanahisi: Mungu hufanya kazi hii vizuri sana, ni faida kwa binadamu na inaweza kuwabadilisha watu. Hata hivyo, hakuna mtu hata mmoja ambaye huhisi kwamba Mungu Amefanya kazi Yake vizuri sana, kwa umuhimu mkubwa sana, na kwamba upendo Wake kwa binadamu ni wa kina sana, na kwamba kwa kweli hajawahi kushughulika na watu kama uchafu usioweza kuvumilika. Watu hawajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu, lakini Mungu amewachukulia watu kama watu. Sivyo ilivyo? Mungu husema kwamba nyinyi ni wanyama, lakini Hajawahi kiwachukulia nyinyi kama wanyama. Ikiwa Angewachukulia kama wanyama, basi kwa nini Awapatie ukweli? Angekuwa Anakuokoa kwa ajili ya nini? Baadhi ya watu wanahisi wamekosewa sana na wanasema: "Mungu Alisema mimi ni mzururaji, nimeaibika sana siwezi kuendelea kuishi." Kwa kweli watu hawaelewi mapenzi ya Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba unaweza kupitia uzoefu wa hekima na makusudi mema ya kazi ya Mungu katika maisha yako yote lakini hutaweza kuyaelewa kwa kina sana. Bila kujali kama uzoefu wako ni wa kina au la almradi mwishoni unaelewa na unajua kidogo, basi hiyo inatosha. Mungu anawaomba watu kuuelewa ukweli na kujikita katika kubadilisha tabia zao, ili polepole kuingia kwa kina katika kujitoa kwao na kujinyenyekeza vilevile katika upendo walio nao kwa Mungu katika mioyo yao. Watu wanapojitolea mhanga kidogo na kupata shida kidogo, basi wanafikiri kwamba michango yao ni mikubwa sana mbele ya Mungu, na kwamba wana ukuu. Wanapofanya mchango wao mdogo, wanakoga ukuu wao, na kama hawataji michango yao, basi hawahisi wapo imara au wametulia. Je, watu wana upendo? Watu wana upendo gani? Je, Mungu hupokea upendo wa kweli wa watu? Je, Mungu si mwenye kustahili upendo wa watu?
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Ijumaa, 25 Januari 2019

Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Sura ya 28. Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kutoa kwenu "muhtasari kuhusu ukweli" hakufanywi ili kuwawezesha watu kupata maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunafanywa ili watu waweze kuwa weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka kwa ukweli. Wao huonekana kana kwamba wanaelewa lengo lililokusudiwa katika kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno ya mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli, na si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Wewe unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na hivyo unapata umiliki wa kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini huwaje unapomaliza kusema? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu na hawana ufahamu wao wenyewe pia. Mwishowe, vitu vyote watakavyokuwa wamepata ni fomyula na sheria, na wanaweza kuzungumza juu ya mambo hayo lakini hakuna kitu kingine, hivyo kama Mungu akifanya jambo jipya, je, mafundisho yote unayoyajua yanaweza kufanana na kile Mungu anachofanya? Kwa hiyo, mambo hayo yako ni sheria tu na wewe unawafanya watu wajifunze theolojia tu: Wewe huwaruhusu kupitia neno la Mungu au kupitia ukweli. Vitabu hivi ambavyo watu hukusanya vinaweza kuwaletea teolojia na ujuzi tu, katika fomyula mpya na katika sheria na mila. Haviwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, au kuwaruhusu watu kuuelewa ukweli au kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Kwa kuuliza swali baada ya swali kuhusu maneno hayo, kisha kujibu, kufanya muhtasari, unadhani kuwa wale walio chini wanaweza kuelewa kwa urahisi. Mbali na kuwa rahisi kukumbuka, wao wana uhakika juu ya maswali haya kwa tazamo la haraka, na unafikiri ni vizuri kufanya mambo kwa njia hii. Lakini kile wanachokielewa siyo maana iliyokusudiwa ya ukweli; inatofautiana na ukweli na ni maneno ya mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Unafanya mambo haya kuwaongoza watu kuelewa ujuzi na weledi wa elimu. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate Mungu na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, si wewe ni sawa tu na Paulo? Ninyi hufikiri kwamba kupata weledi wa ujuzi wa ukweli ni muhimu hasa, na pia kujifunza kwa moyo mafungu mengi ya maneno ya Mungu. Lakini jinsi watu wanavyoelewa neno la Mungu si muhimu hata kidogo. Ninyi hudhani ni muhimu sana kwa watu kuweza kukariri mengi ya maneno ya Mungu, kuweza kuzungumza mafundisho mengi na kugundua fomyula nyingi ndani ya maneno ya Mungu. Kwa hiyo, siku zote ninyi hutaka kuweka katika mfumo vitu hivi ili kila mtu awe akiimba wimbo mmoja na kusema mambo hayo hayo, ili kila mtu aongee mafundisho sawa na wengine, awe na maarifa sawa na huweka sheria sawa—hili ndilo lengo lenu. Ninyi hufanya hivi kana kwamba kuwafanya watu waelewe vizuri zaidi, wakati kwa kinyume chake hamjui kwamba kwa kufanya hivi mnawaingiza watu katikati ya sheria ambazo ziko nje ya ukweli wa maneno ya Mungu. Ili kuwafanya watu wawe na ufahamu halisi wa ukweli, ni lazima ujiunge na uhalisi, jiunge na kazi, na uwalete watu mbele ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ambapo watu wanaweza kuwa na weledi wa ukweli. Ikiwa jitihada zako zinaelekezwa tu kwa kutumia fomyula na sheria kwa maneno yaliyoandikwa, basi hutaweza kufikia ufahamu wa kweli, hutaweza kuwaongoza wengine kwa uhalisi, na seuze kuweza kuwaruhusu wengine kupitia mabadiliko zaidi au kujielewa wenyewe zaidi. Kama neno lililoandikwa lingekuwa badala ya watu, basi hamngehitaji kufanya chochote kamwe.
Nyinyi bado hamjagundua sheria za maneno ya Mungu, na watu wengi husema hivi: "Hakuna mantiki kwa maneno ya Mungu. Kila makala ina ya maudhui ya aina zote na kuna maana tofauti katika kila kifungu na kila sentensi hali inayofanya kuwa vigumu kwetu kukumbuka na vigumu kuelewa. Hata siyo rahisi kufupisha wazo la jumla la ibara." Neno la Mungu siyo riwaya, wala si nadhari au kazi ya fasihi. Ni ukweli; ni neno ambalo humpa mtu uzima. Neno silo jambo ambalo linaweza kueleweka kwa kufikiriwa kwa akili zenu, wala sheria zake haziwezi kufupishwa kwa juhudi kidogo. Kwa hiyo bila kujali ni kipengele kipi watu wana ufahamu mdogo wacho au wana ufahamu wa sheria zake, inaweza tu kuwa ufahamu wa upande mmoja, wa juu juu tu, kama tone moja tu katika bahari, na kimsingi hauwezi kufikia kile alichokusudia Mungu awali. Makala yoyote ya maneno ya Mungu itakuwa na vipengele kadhaa vya ukweli. Kwa mfano, makala kuhusu fumbo la Mungu kupata mwili itajumuisha umuhimu wa kupata mwili pamoja na kazi inayofanywa na upataji wa mwili. Na pia itakuwa na jinsi watu wanavyopaswa kuamini katika Mungu, na labda inaweza pia kuwa na jinsi watu wanavyopaswa kumwelewa na kumpenda Mungu; itajumuisha mambo mengi ya ukweli. Kama, kwa mujibu wa mawazo yako, umuhimu wa kupata mwili ulikuwa na vipengele vichache tu na unaweza kujumlishwa katika sentensi chache, ni matokeo yapi ambayo kazi ya Mungu kwa mtu yangeweza kufanikisha? Watu hufanywa kuelewa umuhimu wa kupata mwili ili kuwafanya wamwelewe Mungu. Baada ya mtu kumwelewa Mungu, kwa kawaida anakuwa na moyo ambao humcha Mungu, na hili sasa linahusisha matendo ya mtu. Hivyo hakuna kipengele cha maneno ya Mungu na hakuna kipengele cha ukweli kilicho rahisi kama unavyofikiria. Ikiwa wewe hutazama neno la Mungu na lugha ya Mungu kuwa rahisi, ukifikiri kwamba swali lolote linaweza kujibiwa kwa ibara ya maneno ya Mungu, basi huo si ukweli. Kila makala ina mitazamo mingi ambayo maneno ya Mungu huzungumzwa kwayo na hakuna njia ya watu kufupisha au ya kutoa muhtasari wa maneno Yake. Baada ya kufupisha maneno Yake, unafikiri fungu hili limejibu swali lililo hapo juu, lakini fungu hili pia linahusiana na maswali mengine. Kwa hiyo unasema nini kwa hilo? Ukweli una mambo mengi. Kwa nini husemwa kuwa ukweli ni uzima, kwamba unaweza kuleta starehe kwa mtu, kwamba hauwezi kupitiwa kwa ukamilifu wake kwa aushi kadhaa au miaka mia kadhaa? Kwa mfano ulikuwa uvitolee muhtasari baadhi ya vipengele vya ukweli au kifungu fulani cha maneno ya Mungu, halafu uulize swali kulihusu hilo. Kisha, kuzingatia swali hili, ulikuwa usome kifungu hiki, kisha ingekuwa dhahiri kuwa hiki kifungu kimesomwa kwa kulijibu swali hilo. Kwa hiyo kifungu hiki kimekuwa fomyula, kanuni na mafundisho, na si ukweli. Ingawa hakuna hata moja ya maneno ya awali limebadilika, hiki kwa dhahiri sana ni kipande cha mafundisho, na sio ukweli. Kwa nini? Kwa sababu swali ulilouliza uliliuliza vibaya. Liliwaongoza watu kupotea na kuwaingiza katika mafundisho, likawafanya kufikiri, kuwaza, kufikiria swali hili, na walisoma kifungu hiki kwa mujibu wa mafundisho yako, kukisoma wakitumia mtazamo wako wa mafundisho. Kisha wangekisoma tena na kurudia, wakiona swali moja pekee na bila kuona kitu kingine chochote. Mwishowe wao wangeletwa mahali ambapo hawawezi kupata ukweli na hawawezi kupitia neno la Mungu, mahali ambapo wanaweza kujiandaa tu na kujadili mafundisho na ni mahali ambapo hawawezi kumwelewa Mungu. Yote ambayo wangeweza kuzungumza yangekuwa mafundisho yenye kupendeza, mafundisho sahihi, lakini hakungekuwa na uhalisi ndani yao na hawangekuwa na njia ya kutembelea. Aina hii ya kuongoza kweli hufanya madhara makubwa!
Ni nini mwiko mkubwa katika huduma ya mtu kwa Mungu? Unajua? Wale miongoni mwenu ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli mlivyo na uwezo. Hata hivyo, nyinyi hamzingatii kufahamu ukweli na kuingia katika uhalisi wa neno la Mungu. Nyinyi daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi? Wengine hata husema: "Kwa kufanya hivi nina uhakika kwamba Mungu atafurahi sana; Yeye kweli atapenda sana. Wakati huu nitaacha Mungu aone, kumpa Yeye mshangao mzuri." Kwa sababu yashangao huu unaondolewa! Usifanye tu chochote kijacho akilini mwako bila kufikiri. Je, inawezaje kuwa sawa kutozingatia matokeo hayo? Wakati wale kati yenu ambao huudhi tabia ya Mungu na kuziudhi amri Zake za utawala wataondolewa wakati huo, hakutakuwa na maneno mnayoweza kusema. Bila kujali dhamira yako, bila kujali kama wewe hufanya hivyo kwa makusudi au la, kama wewe huelewi tabia ya Mungu au huyaelewi mapenzi ya Mungu, kwa urahisi utamkosea Mungu na kwa urahisi utaziudhi amri Zake za utawala, hiki ni kitu ambacho kila mtu ni lazima ajichunge dhidi yake. Mara unapoziudhi amri za utawala za Mungu au kuiudhi tabia ya Mungu, Mungu hataangalia kama ulifanya hivyo makusudi au bila kukusudia; hiki ni kitu ambacho ni lazima uone kwa dhahiri. Ikiwa huwezi kuona ukweli halisi wa suala hili, basi unahakikishiwa kuwa na tatizo. Katika kumhudumia Mungu, watu wanataka kupiga hatua kubwa, kufanya mambo makubwa, kusema maneno makubwa, kufanya kazi kubwa, kuchapisha vitabu vikubwa, kufanya mikutano mikubwa na kuwa viongozi wakuu. Kama siku zote una matarajio makuu, basi utaziudhi amri kuu za utawala za Mungu; watu kama hawa watakufa haraka. Kama wewe si mwenye tabia njema, mwenye kumcha Mungu au mwenye busara katika kumhudumia Mungu, ipo siku utaziudhi amri za utawala za Mungu. Kama ukikosea tabia ya Mungu, kuziudhi amri Zake za kiutawala, na hivyo kutenda dhambi dhidi ya Mungu, basi Yeye hataangalia kuona ni kwa sababu gani ulitenda hivi, wala kuona nia zako. Kwa hivyo unafikiri Mungu hana busara? Je, Yeye amekosa huruma kwa mwanadamu? Hapana. Kwa nini Mimi Ninasema hapana? Kwa sababu watu si kiziwi, mjinga au kipofu. Nyote mnaweza kuona na kusikia, na bado mnasababisha kosa. Ni sababu gani unaweza kuizungumzia bado? Hata kama wewe huhifadhi nia zozote, mara unapokosea Mungu, lazima utaangamia na kupata adhabu. Kuna haja ya hali yoyote yako izingatiwe? Hakuna mtu yeyote anayelazimishwa kwa kisu kuzikosea amri za utawala za Mungu au tabia ya Mungu. Hili halifanyiki kamwe. Mtu alikuwekea kisu kooni na kukulazimisha, akisema: "Mlaani Mungu wenu. Baada ya kumlaani Yeye nitakupa pesa na sitakuua." Labda katika hali aina hii ungesema maneno ya kukufuru kwa sababu tu unaogopa kufa. Je, hali ya aina hii inaweza kutokea? Mambo huwa hayafiki kiwango hiki, ama hufika? Kwamba tabia ya Mungu haitaruhusu kosa ina maana yake iliyodokezwa. Hata hivyo adhabu za Mungu zinategemeza hali za watu na asili zao. Hali moja ni pale ambapo mtu hajui kuwa Yeye ni Mungu naye humkosea Yeye. Kujua kwamba Yeye ni Mungu na bado kumkosea Yeye kwa makusudi ni hali nyingine. Ikiwa mtu anafahamu kikamilifu kwamba Yeye ni Mungu na bado humkosea, basi mtu huyo ni lazima aadhibiwe. Mungu huonyesha kiasi cha tabia Yake katika kila hatua ya kazi Yake—watu wanafahamu chochote kwa hili? Katika siku za mwisho, Mungu amefanya kazi kwa miaka mingi, je, watu hawajui tabia Yake na ni vitu vipi ambavyo watu hufanya au kusema ambavyo vinaweza kumchukiza Mungu kwa urahisi? Na vitu ambavyo vimefafanuliwa na amri za utawala za Mungu—kile watu wanapaswa kufanya na kile hawapaswi kufanya—Je, watu hawajui hayo pia? Watu hawawezi kuelewa mambo fulani ambayo yanahusiana na ukweli au na kanuni. Hiyo ni kwa sababu hawajapitia kufikia kiwango hicho, na hivyo hawana njia ya kuelewa. Lakini amri za utawala za Mungu ziko ndani ya mawanda yaliyofafanuliwa na yanastahili kuwa ya sheria. Sio lazima kwa watu kuzielewa kwa njia yoyote, ni kwamba tu wafuate maana yazo halisi. Je, si hili ni jambo ambalo mtu sharti apambane nalo? Wewe huzingatii zaidi kitu chochote na humwogopi Mungu, kwa hiyo ni lazima upate adhabu!
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Alhamisi, 24 Januari 2019

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Kote katika ulimwengu mkubwa mno, sayari zote ya mbingu husogea kwa usahihi katika mizunguko yazo zenyewe. Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Hili lote limepangwa vizuri sana—je, kuna Mwenye Uwezo Mmoja anayepanga na kutawala yote haya? Tangu tuje katika ulimwengu huu tukilia tumeanza kutekeleza majukumu tofauti katika maisha. Sisi husogea kutoka kuzaliwa mpaka uzee mpaka kuugua hadi kifo, sisi husogea kati ya furaha na huzuni…. Wanadamu kwa kweli hutoka wapi, na kwa kweli tutaenda wapi? Ni nani huitawala jaala yetu? Kutoka nyakati za kale hadi siku za kisasa, mataifa makubwa yameibuka, nasaba za wafalme zimekuja na kwenda, na nchi na watu wamesitawi na kuangamia katika mikondo ya historia…. Kama tu sheria za asili, sheria za maendeleo ya wanadamu zina mafumbo yasiyo na kikomo. Ungependa kujua majibu kuyahusu? Filamu iitwayo Yule Ambaye Hushikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu itakuongoza kufikia kiini cha jambo hili, ili kufichua mafumbo yote haya!
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Jumatano, 23 Januari 2019

Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

 bhvViumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu

I
Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye hufanya viumbe vyote kuja chini ya amri Yake, na kutii utawala Wake. Anaamuru vitu vyote, akividhibiti katika mikono Yake. Vitu hai, milima, mito na mwanadamu lazima vyote vije chini ya amri Yake. Vitu angani na duniani lazima vyote vije chini ya utawala Wake. Vyote lazima vitii, bila uchaguzi wowote. Hii ni amri ya Mungu na mamlaka Yake.
II
Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye hufanya viumbe vyote kuja chini ya amri Yake, na kutii utawala Wake. Kila kitu kinaamuriwa na Mungu. Anaamuru na kuvipanga vitu vyote, kila kuainishwa kulingana na aina na kwa mapenzi ya Mungu kupewa nafasi yake. Vitu angani na duniani lazima vyote vije chini ya utawala Wake. Vyote lazima vitii, bila uchaguzi wowote. Hii ni amri ya Mungu na mamlaka Yake.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumanne, 22 Januari 2019

Kutupa mbali Jozi La Shetani Kunakomboa

Kutupa mbali Jozi La Shetani Kunakomboa

Momo Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui
Kabla ya kumwamini Mungu, bila kujali chochote nilichokuwa nikifanya, sikuwahi kutaka kubaki nyuma. Nilikuwa tayari kukubali shida yoyote ili mradi ingemaanisha ningeinuka juu ya kila mtu mwingine zaidi. Baada ya kumkubali Mungu, mtazamo wangu uliendelea kuwa sawa, kwa sababu niliamini kikamilifu msemo, “Hakuna maumivu, hakuna faida,” na kuona mtazamo wangu kama ushahidi wa msukumo wangu. Wakati Mungu alinifichulia ukweli, hatimaye niligundua kuwa nilikuwa nikiishi chini ya jozi la Shetani, nikiishi chini ya miliki yake.
Sio muda mrefu sana uliopita, kanisa lilifanya mipango ya kumtuma dada niliyeshiriki naye ili aweze kuhudumu katika nafasi ya uongozi. Niliposikia habari hizo, nilisononeka. Sisi sote tulikuwa tunahudumu katika majukumu ya uongozi hadi tulipoteuliwa tena kama wahariri. Sasa dada yangu angerudia nafasi ya uongozi na kumtumikia Mungu akiwa na uwezekano usio na kikomo wa ukuaji, lakini bado ningebakia nikifanya kazi kwa dawati, nikitekeleza kazi yangu bila kuonekana. Kunaweza kuwa na mategemeo gani ya baadaye katika hayo? Kwa kubadili mawazo, nilikumbushwa msemo wa kale, “Kuna njia milioni tofauti za mafanikio.” Ili mradi ningekamilisha kazi yangu vizuri, ningeweza pia kufanikiwa. Nilihitaji tu kuzidisha jitihada zangu katika kutafuatilia ukweli. Ikiwa ningelenga kuhariri mahubiri ili yawasilishe ukweli vizuri zaidi, labda siku moja viongozi wangeona kuwa nilielewa ukweli. Kisha wangenipandisha cheo na siku zangu za baadaye zingekuwa pia za kuchangamsha. Baada ya utambuzi huu, mawingu ya kijivu yalianza kurejea kwa ajili ya uamuzi mpya. Nilijitosa katika kazi yangu, na nikala na kunywa neno la Mungu wakati sikuwa na shughuli, bila kuthubutu kulegea hata kwa muda.
Siku moja, niliona kifungu kinachofuata katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha: “Kila kitu kinachokuzuia kumtafuta Mungu na kutafuta ukweli ni mojawapo ya pingu za Shetani. Ukiwa umefungwa na moja kati ya minyororo ya Shetani, unaishi maisha yako chini ya miliki yake.” Baada ya kusikia haya, sikuweza kujizuia ila kuuliza, “Ni ipi kati ya jozi za shetani ninayoishi chini yake? Ni ipi kati ya sumu zake inayozuia utafutiliaji wangu wa ukweli?” Nilipojaribu kutafakari swali hili kwa kimya, nilikumbushwa hali yangu ya hivi karibuni. Baada ya dada yangu kupelekwa kwenye daraja lake jipya, sikuwa wa kutoonyesha hisia. Kwa kweli, nilijitolea zaidi kula na kunywa neno la Mungu, kumwomba Mungu, na kutekeleza kikamilifu kazi yangu. Kijuujuu, nilionekana kuwa na bidii zaidi katika kutafuta ukweli kuliko hapo awali, lakini ukifunua pazia na kuichambua, uwezo wangu wa kukubali kubaki nyuma ni kwa sababu nilikuwa na matamanio ya kuendelea siku moja. Tamaa yangu ya kuchochea kuwa bora zaidi ilikuwa ndiyo sababu sikuwa wa kutoonyesha hisia na badala yake nilifuatilia ukweli zaidi mno, lakini kunakodhaniwa kuwa ufuatiliaji wangu wa ukweli kulikuwa tu njonzi, ufuatiliaji ulio mchafu. Nilikuwa nikishiriki ufuatiliaji wa muda wa ukweli ili kutimiza madhumuni yangu ya kibinafsi. Nikifikiri nyuma kwa miaka yangu iliyotumika kufuata Mungu, nilitambua kuwa dhabihu zangu zote zilikuwa zimelipwa na sumu ya Shetani “Hakuna maumivu, hakuna faida.” Hivi ndivyo ilivyonifunga pingu isiyoonekana na kunitia kujitahidi kwa ubora. Nilipokuwa na cheo tayari, nilikuwa bado nikitafuta hata cha juu zaidi; Nilipopoteza cheo changu au niliposhindwa kujiendeleza, sikuwa wa kutoonyesha hisia; Mimi bado nilionekana kuwa na hiari ya kulipa bei ili kutafuta ukweli. Hata hivyo, hii haikuwa kwa sababu nilielewa ukweli na nilikuwa tayari kujitoa mhanga kwa ajili yake. Nilitaka tu kutumia kuonekana kwa kujitoa mhanga kwa jitihada za kufanikiwa. Hapo ndipo nilipobaini hatimaye kuwa msimamo wangu wa “Hakuna maumivu, hakuna faida,” ulikuwa kweli mojawapo wa sumu za Shetani zilizokuwa zikitiririka kupitia mishipa yangu. Nilikuwa nimetanganywa; sumu ilikuwa imeninyonya ubinadamu wangu wote. Nilikuwa na kiburi na mwenye tamaa bila hisia yoyote ya taswira yoyote. Mambo hayo yote yalifanyika kabisa chini ya pua langu. Kwa kweli nilifikiri kuwa matamanio yangu yalikuwa ushuhuda wa matarajio yangu. Nilidhani kuwa hali yangu ya kiburi ya kutotaka kubaki nyuma ilikuwa ishara ya motisha yangu. Niliabudu uongo wa Shetani kama ukweli na kuuona kama beji ya heshima badala ya alama ya fedheha. Nilikuwa mjinga kiasi kipi hadi kudanganyika na Shetani kiasi kile, kutojua kutofautisha kati mema na uovu? Hatimaye niliona jinsi nilivyokuwa ovyo. Nilijifunza pia jinsi Shetani ni mwenye kudhuru kwa siri na mwenye kuleta hizaya. Shetani hutumia udanganyifu spesheli kutudanganya na kutupotosha. Hutupotosha, na tunaapa uaminifu kwa mipango yake danganyifu. Hii yote hufanywa bila ujuzi wetu. Tunadhani tunatafuta ukweli na kujitolea kwa ajili ya kweli, lakini kwa kweli tunaishi katika kujidanganya. Sumu za Shetani zina nguvu kabisa! Ikiwa haingekuwa nuru yake Mungu, singewahi kamwe kuona ukweli kwamba nilikuwa nimepotoshwa na Shetani, na hakika singeweza kamwe kubaini mipango yake ya udanganyifu. Ikiwa haingekuwa nuru ya Mungu, ningeendelea kuishi chini ya jozi la Shetani, hadi wakati Shetani hatimaye anitumie mzima.
Wakati huo, nilifikiria kuhusu maneno ya Mungu: “Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mtiifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu” (“Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinionyesha njia ya kutenda: Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, napaswa kumpenda na kumridhisha bila masharti na kutekeleza wajibu wangu kwa dhati. Hii ndiyo hisi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kumiliki. Huu ni ufuatiliaji ambao unaambatana na mapenzi Yake. Kuanzia siku ya leo kwenda mbele, nitafanya liwezekanalo kufuatilia ukweli. Nitategemea ukweli ili kupenya udanganyifu wa Shetani na kutupa jozi lake. Sitafuatilia tena kitu chochote cha mwili. Badala yake, nitafanya kazi kwa bidii kwa kutoonekana, kutimiza wajibu wangu kumkidhi Mungu. Hata nikiachwa bila kitu chochote mwishowe, nitaendelea kwa hiari bila majuto yoyote, kwa sababu mimi ni moja tu wa viumbe duni wa Mungu. Kumridhisha Muumba ni nia yangu moja ya kweli maishani.
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Vitabu.

Jumatatu, 21 Januari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" Sehemu ya Kwanza

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kuhusu Majina na Utambulisho" Sehemu ya Kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, "Yesu aliwakilisha Roho wa Mungu, na Alikuwa Roho wa Mungu Akifanya kazi moja kwa moja. Alifanya kazi ya enzi mpya, kazi ambayo hakuna aliyekuwa amefanya mbeleni. Yeye Alifungua njia mpya, Alimwakilisha Yehova, na Alimwakilisha Mungu Mwenyewe. Ilhali kwa Petro, Paulo na Daudi, bila kujali walichoitwa, waliwakilisha tu utambulisho wa kiumbe wa Mungu, ama walitumwa na Yesu na Yehova. Kwa hivyo bila kujali kiasi cha kazi walichofanya, bila kujali jinsi walivyofanya miujiza kubwa, walikuwa bado tu viumbe wa Mungu, na hawakuweza kuwakilisha Roho Mtakatifu. Walifanya kazi kwa jina la Mungu ama baada ya kutumwa na Mungu; zaidi ya hayo, walifanya kazi katika enzi iliyoanzishwa na Yesu ama Yehova, na kazi waliyoifanya haikutengwa. Walikuwa, hatimaye, viumbe wa Mungu tu."

Jumapili, 20 Januari 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Bila kazi ya Yesu, mwanadamu hangeweza kushuka chini kutoka msalabani, lakini bila kupata mwili siku hii, wale wanaoshuka chini kutoka msalabani hawangewahi kusifiwa na Mungu ama kuingia katika enzi mpya. Bila kuja kwa huyu mwanadamu wa kawaida, basi hamngeweza kuwa na hii fursa ama kustahiki kuona uso wa ukweli wa Mungu, kwani nyinyi nyote ni wale ambao wangepaswa kuangamizwa kitambo sana. Kwa sababu ya kuja kwa Mungu mwenye mwili kwa mara ya pili, Mungu amewasamehe na kuwaonyesha huruma. Bila kujali, maneno ambayo lazima Niwaachie mwishowe ni haya: Huyu mwanadamu wa kawaida, ambaye ni Mungu mwenye mwili, ni wa umuhimu sana kwenu. Hili ndilo jambo kubwa ambalo Mungu tayari Amefanya miongoni mwa wanadamu."