Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumapili, 30 Septemba 2018

Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)

Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)

Safi na mwaminifu kama mtoto, asiye na hatia na mchangamfu, aliyejawa na nguvu za ujana, wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni. Hakuna uongo, udanganyifu au hadaa, na moyo ulio wazi na mwaminifu, wanaishi na heshima. Wanaitoa mioyo yao kwa Mungu, Mungu anawaamini, na wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda.
Wale wanaopenda ukweli wote wana mioyo ya uaminifu. Watu waaminifu hufurahia kutenda ukweli, na kwa kumtii Mungu mioyo yao ina amani. Wanamcha Mungu, wanaepuka maovu na wanaishi kulingana na maneno ya Mungu. Wanaishi katika maneno ya Mungu na wamewekwa huru na kuachiliwa. Wanakubali uchunguzi wa Mungu na kuishi mbele Yake. Kumpenda Mungu ni kuwa na furaha na mwenye shangwe.
Ndugu, tumemwamini Mungu tangu tulipokuwa wadogo. Je, tuna furaha? Ndiyo, tuna furaha! Nina furaha pia!
Ninapompenda Mungu, moyo wangu una utulivu na una furaha, na ninaishi kwa urahisi ninapotenda kulingana na maneno ya Mungu. Moyoni mwangu kuna Mungu tu, kuna ukweli tu, maneno ya Mungu yamekuwa maisha yangu. Nikiishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu kila siku, ninabarikiwa na Mungu na Roho Mtakatifu ananiongoza. Wanakubali uchunguzi wa Mungu na kuishi mbele Yake. Kumpenda Mungu ni kuwa na furaha na mwenye shangwe. Nikiishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu kila siku, ninabarikiwa na Mungu na Roho Mtakatifu ananiongoza. Ufalme wa Kristo ni mbinguni kwa watu waaminifu, na ni makao yao ya kupendeza.
kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wimbo wa Kikristo

Jumamosi, 29 Septemba 2018

Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God


Swahili Christian Song "Matendo ya Mungu Yanajaza Ulimwengu Mzima Tupu" | Praise the Great Power of God

Mungu anatazama chini juu ya vitu vyote kutoka juu, na Anatawala vitu vyote kutoka juu. Wakati huo huo, Mungu ametuma wokovu Wake juu ya dunia. Mungu anaangalia kutoka mahali Pake pa siri kila wakati, kila hatua ya mwanadamu, kila kitu anachosema na kufanya.
Mungu anamjua mwanadamu kama kiganja cha mkono Wake. Mahali pa siri ni makao ya Mungu, anga ndicho kitanda Mungu akilaliacho. Nguvu ya Shetani haiwezi kumfikia Mungu, kwani Yeye amejawa na utukufu, haki, na hukumu.
Mungu amekanyaga vitu vyote na miguu Yake, Yeye ananyosha mtazamo Wake juu ya ulimwengu. Na Mungu ametembea kati ya wanadamu, ameonja utamu na uchungu, ladha zote za dunia ya mwanadamu; lakini wanadamu, kamwe hawakumtambua Mungu kweli, wala hawakumwona Mungu alipokuwa akitembea ughaibuni. Kwa sababu Mungu alikuwa kimya, na hakufanya matendo yasiyo ya kawaida, hivyo, hakuna aliyemwona kweli. Vitu haviko vilivyokuwa awali: Mungu anaenda kufanya vitu ambavyo, katika enzi zote, ulimwengu haujawahi kuona, Mungu anaenda kunena maneno ambayo, katika enzi zote, wanadamu hawajawahi kusikia, kwa sababu Yeye anawataka binadamu wote waje kumjua Mungu katika mwili. kwa sababu Yeye anawataka binadamu wote waje kumjua Mungu katika mwili.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kazi ya Mungu

Alhamisi, 27 Septemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maneno kwa Vijana na Wazee

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, neno la Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maneno kwa Vijana na Wazee

Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya.

Jumatano, 26 Septemba 2018

Neno la Mungu | "Kazi katika Enzi ya Sheria" | How Did God Guide the Original Mankind?

Neno la Mungu | "Kazi katika Enzi ya Sheria" | How Did God Guide the Original Mankind?

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Kwenye Enzi ya Sheria, Yehova Aliweza kuweka wazi sheria nyingi kwa Musa kupitisha kwa wana wa Israeli waliomfuata kutoka Misri. … Yehova Alianzisha sheria Zake na taratibu ili huku Akiyaongoza maisha yao, watu wangeweza kumsikiliza na kuheshimu neno Lake na wala si kuasi neno Lake. Alitumia sheria hizi kuweza kudhibiti kizazi kipya cha binadamu kilichozaliwa, kuweka msingi wa kazi Yake ambayo ingefuata. Na kwa hivyo, sababu ya kazi ambayo Yehova Alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya Sheria."
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumfuata Mungu

Jumanne, 25 Septemba 2018

Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Mazungumzo Mafupi Kuhusu 'Ufalme wa Milenia Umefika'"

Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Mazungumzo Mafupi Kuhusu 'Ufalme wa Milenia Umefika'"

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, watu tayari watakuwa wamefanywa wakamilifu, na tabia mbovu ndani yao zitakuwa zimetakaswa. Wakati huo, maneno yasemwayo na Mungu yatawaongoza wanadamu hatua kwa hatua, na kufichua siri za kazi ya Mungu tangu uumbaji hadi leo, na maneno Yake yatawaambia watu kuhusu matendo ya Mungu katika kila enzi na kila siku, jinsi Anavyowaongoza watu ndani, kazi Aifanyayo katika ufalme wa kiroho, na yatawaambia watu kuhusu mienendo ya ufalme wa kiroho. Hapo tu ndipo itakuwa Enzi ya kikweli ya Neno; kwa sasa ni mfano tu."
Soma Zaidi:  Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Tafuta Ufalme wa Mungu Kwanza

Jumatatu, 24 Septemba 2018

Neno la Mungu "Jinsi ya Kuujua Uhalisi"

Neno la Mungu "Jinsi ya Kuujua Uhalisi"

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi, ndivyo wanavyokuwa na dhana kidogo zaidi; kadiri watu wanavyopitia uhalisi zaidi, kadiri wanavyojua zaidi matendo ya Mungu wa uhalisi, na ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kuacha nyuma tabia zao potovu na za kishetani; kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyomjua Mungu zaidi na kuuchukia mwili zaidi na kupenda ukweli; na kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyofika karibu na ubora wa mahitaji ya Mungu."
Soma Zaidi:  Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu

Jumapili, 23 Septemba 2018

Umeme wa Mashariki | Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, makusudi ya Mungu

Umeme wa Mashariki | Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Qingxin Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Kuhusu kipengele cha ukweli cha "Mungu ni mwenye haki ", siku zote nilikuwa na ufahamu wa upuuzi kwa kiasi fulani. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa,

Jumamosi, 22 Septemba 2018

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Pitia Hukumu Katika Siku za Mwisho na Upite Katika Mtego wa Shetani

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Pitia Hukumu Katika Siku za Mwisho na Upite Katika Mtego wa Shetani

Biblia inasema, "Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu..." (1 Petro 4:17). Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli wote unaomtakasa na kumwokoa mwanadamu na Anatuonyesha tabia Yake yenye haki, uadhama na isiyokosewa. Kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho imefanywa kumwokoa mwanadamu ili aweze kujinasua kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kurudi kwa Mungu. Watu wote wateule wa Mungu ambao wanakubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu wote polepole huja kuona wazi ukweli wa ukweli kwamba huduma ya wachungaji na wazee kwa Mungu kwa kweli humkataa Mungu, kuona wazi asili zao za unafiki na upinga Kristo na kuchukia ukweli na kwa hivyo kujinasua kutoka kwa kuchanganyikiwa na udhibiti wa wachungaji na wazee na kurudi kwa kweli mbele ya Mungu. Kwa kusikiliza ushuhuda wa uzoefu wa hukumu mbele ya kiti cha Kristo wa watu wateule wa Mungu, utaletwa kwa ufahamu wa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho.
Sikiliza zaidi: Umeme wa Mashariki video
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Sinema za Injili

Ijumaa, 21 Septemba 2018

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini?

Filamu za Injili | "Kupita Katika Mtego" | Mtu Anaweza Kuokolewa kwa Kumwamini Bwana Katika Dini?

Ndani ya dini, kuna watu wengi ambao wanaamini kwamba, ingawa wachungaji na wazee wanashikilia mamlaka katika ulimwengu wa dini na kutembea njia ya Mafarisayo wafiki, ingawa wanakubali na kuwafuata wachungaji na wazee, wanaamini katika Bwana Yesu, si katika wachungaji na wazee, hivyo basi inawezaje kusemwa kuwa njia wanayoyotembea pia ni ile ya Mafarisayo? Je, mtu kweli hawezi kuokolewa kwa kumwamini Mungu ndani ya dini?
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Alhamisi, 20 Septemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuzaliwa Upya Kupitia Neno la Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kukamilishwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 92. Kuzaliwa Upya Kupitia Neno la Mungu

Wang Gang Mkoa wa Shandong
Mimi ni mkulima na kwa sababu familia yangu ni maskini, daima ilinibidi nisafiri kwenda kote kutafuta kazi za muda ili kupata pesa; nilidhani kuwa ningeweza kujipatia maisha mazuri kupitia kazi yangu ya kimwili.

Jumatano, 19 Septemba 2018

Swahili Christian Variety Show | "Mchungaji wetu alisema …" (Mazungumzo Chekeshi)

Swahili Christian Variety Show | "Mchungaji wetu alisema …" (Mazungumzo Chekeshi)

Yu Shunfu ni muumini katika ulimwengu wa dini ambaye huenzi na huabudu wachungaji na wazee wa kanisa. Yeye hufikiri "wachungaji na wazee wa kanisa wote walikuzwa na Mungu, na kutii wachungaji na wazee wa kanisa ni kutii Mungu, "kwa hivyo yeye humsikiza mchungaji wake katika yote anayofanya, hata katika mambo ya kukaribisha kuja kwake Bwana. Lakini kupitia kwa mjadala mzuri sana, Yu Shunfu amekuja kuona kuwa kuzingatia dhana za dini ni upuzi na upumbavu, na mwishowe anagundua kuwa kumtukuza Mungu huja kwanza katika imani, na kwamba lazima yeyote asetiri "hekalu" la moyo kwa ajili ya Mungu. Kwa hivyo, anaamua kutafuta na kuchunguza njia ya ukweli kivyake ...
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, mapenzi ya Mungu

Jumanne, 18 Septemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Mia Moja na Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Mia Moja na Tano

Kwa sababu ya kanuni za maneno Yangu, kwa sababu ya utaratibu wa kazi Yangu, watu hunikana; hili ndilo kusudi Langu la kuzungumza kwa muda mrefu (imezungumzwa kuhusu wazao wote wa joka kubwa jekundu).

Jumatatu, 17 Septemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Kila hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu ina umuhimu wake mkubwa. Yesu alipokuja zamani, Alikuwa mwanaume, lakini Mungu anapokuja wakati huu Yeye ni mwanamke. Kutokana na hili, unaweza kuona kwamba Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke kwa ajili ya kazi Yake na Kwake hakuna tofauti ya jinsia. Roho Wake anapowasili, Anaweza kuchukua mwili wowote kwa matakwa Yake na mwili huo unaweza kumwakilisha Yeye. Uwe wa kiume au kike, unaweza kumwakilisha Mungu alimradi tu ni mwili Wake wa nyama. Kama Yesu angeonekana kama kike alipokuja, kwa maneno mengine, iwapo mtoto wa kike, sio wa kiume, angezaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, hatua hiyo ya kazi ingekuwa imekamilika pia. Kama hali ingekuwa hivyo, basi hatua ya leo ya kazi ingelazimika kukamilishwa badala yake na mwanaume, lakini kazi ingekamilika pia. Kazi inayofanywa katika hatua hizi zote ni muhimu kwa kiwango sawa; hakuna hatua yoyote ya kazi inayojirudia au kupingana na nyingine. Wakati huo, Yesu alipokuwa akifanya kazi Yake aliitwa Mwana wa pekee, na “Mwana” inaashiria jinsia ya kiume. Basi kwa nini Mwana wa pekee halikutajwa katika hatua hii? Hii ni kwa sababu mahitaji ya kazi yamelazimisha badiliko la jinsia ambayo ni tofauti na ile ya Yesu. Kwa Mungu hakuna tofauti ya jinsia. Kazi Yake inafanywa kama Anavyotaka na katika kufanya kazi Yake hazuiliwi na kitu chochote kile, lakini hasa yupo huru. Hata hivyo, kila hatua ya kazi ina umuhimu wake mkubwa. Mungu alipata mwili mara mbili, na ni dhahiri kwamba kupata mwili Kwake katika siku za mwisho ni mara ya mwisho. Amekuja kufichua matendo Yake yote. Ikiwa katika hatua hii Hakupata mwili ili Yeye binafsi afanye kazi kwa ajili ya mwanadamu kushuhudia, mwanadamu milele angeshikilia fikra kwamba Mungu ni wa kuime tu, na si wa kike. Kabla ya hili, wanadamu wote waliamini kwamba Mungu angeweza kuwa tu mwanaume na kwamba mwanamke hawezi kuitwa Mungu, maana wanadamu wote walimchukulia mwanamume kuwa na mamlaka juu ya mwanamke. Waliamini kwamba hakuna mwanamke anayeweza kuchukua mamlaka, bali ni mwanamume tu. Aidha hata walisema kwamba mwanamume alikuwa ni mkuu wa mwanamke na kwamba mwanamke anapaswa kumtii mwanaume na asimshinde. Iliposemwa hapo nyuma kwamba mwanamume alikuwa mkuu wa mwanamke, ilielekezwa kwa Adamu na Hawa ambao walikuwa wamedanganywa na yule nyoka, na wala sio kwa mwanamume na mwanamke kama walivyoumbwa na Yehova hapo mwanzo. Bila shaka, mwanamke anapaswa kumtii na kumpenda mume wake, na mume anapaswa kujifunza kuilisha na kuiruzuku familia yake. Hizi ni sheria na kanuni zilizowekwa na Yehova ambazo kwazo wanadamu wanapaswa kuzifuata katika maisha yao ya hapa duniani. Yehova alimwambia mwanamke “Ashiki yako itakuwa kwa mume wako, na atatawala juu yako.” Alisema hivyo tu ili kwamba wanadamu (yaani, mwanamume na mwanamke) waweze kuishi maisha ya kawaida chini ya utawala wa Yehova, na tu ili kwamba maisha ya wanadamu yaweze kuwa na mfumo na yasipoteze mwelekeo. Kwa hivyo, Yehova alitengeneza kanuni zinazofaa ya namna ambavyo mwanamume na mwanamke wanavyopaswa kutenda, lakini hili lilihusu tu viumbe wote wanaoishi duniani na halikuhusiana na mwili wa Mungu wa nyama. Inawezekanaje Mungu awe sawa na viumbe Wake? Maneno Yake yalielekezwa tu kwa wanadamu wa viumbe Wake; Alianzishia mwanamume na mwanamke kanuni ili wanadamu waweze kuishi maisha ya kawaida. Hapo mwanzo, Yehova alipoumba wanadamu, Aliwaumba wanadamu wa aina mbili, mwanamume na mwanamke; na kwa hiyo, mwili Wake wa nyama pia ulitofautishwa kuwa wa kiume au wa kike. Hakuamua juu kazi Yake kulingana na maneno aliyozungumza kwa Adamu na Hawa. Mara mbili Alipopata mwili kuliamuliwa kwa kuzingatia kabisa mawazo Yake alipowaumba wanadamu kwa mara ya kwanza, yaani, Alikamilisha kazi ya kupata Kwake mwili mara mbili, kwa msingi wa mwanamke na mwanamume kabla ya wao kupotoshwa. Ikiwa wanadamu wangechukua maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Adamu na Hawa ambao walikuwa wamedanganywa na yule nyoka na kuyatumia katika kazi ya mwili wa Mungu, je, si Yesu pia angepaswa kumpenda mke Wake kama Alivyotakiwa? Je, kwa njia hii, Mungu bado ni Mungu? Na ikiwa ni hivyo, je, bado Angeweza kukamilisha kazi Yake? Ikiwa ni vibaya kwa mwili wa Mungu kuwa mwanamke, je, basi lisingekuwa kosa kubwa sana pia kwa Mungu kumuumba mwanamke? Ikiwa mwanadamu bado anaamini kwamba Mungu kupata mwili kama mwanamke ni vibaya, je, basi Yesu, ambaye hakuoa na hivyo hakuweza kumpenda mke Wake, angekuwa na makosa kama kupata mwili wa sasa? Kwa kuwa unatumia maneno yaliyozungumzwa na Yehova kwa Hawa ili kupima ukweli wa Mungu kupata mwili leo, basi unapaswa kutumia maneno ya Yehova kwa Adamu kumhukumu Bwana Yesu ambaye alipata mwili katika Enzi ya Neema. Je, hawa wawili sio sawa? Kwa kuwa unampima Bwana Yesu kulingana na mwanamume ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka, basi hupaswi kuhukumu ukweli wa kupata mwili leo hii kulingana na mwanamke ambaye alikuwa amedanganywa na yule nyoka. Hili si haki! Ikiwa umefanya hukumu ya namna hiyo, inathibitisha kukosa urazini kwako. Yehova alipopata mwili mara mbili, jinsia ya mwili Wake ilikuwa inahusiana na mwanamume na mwanamke ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka; Alipata mwili mara mbili kulingana na mwanamume na mwanamke ambaye hakuwa amedanganywa na yule nyoka. Usifikiri kwamba uanaume wa Yesu ulikuwa sawa na uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka. Hahusiani naye kabisa, na ni wanaume wawili wa asili tofauti. Hakika haiwezi kuwa kwamba uanaume wa Yesu unathibitisha Yeye ni mkuu wa wanawake wote lakini sio mkuu wa wanaume wote? Je, Yeye si Mfalme wa Wayahudi wote (ikiwa ni pamoja na wanaume na wanawake)? Yeye ni Mungu Mwenyewe, sio tu mkuu wa mwanamke bali mkuu wa mwanamume pia. Yeye ni Bwana wa viumbe vyote, na mkuu wa viumbe vyote. Unawezaje kuamua uanaume wa Yesu kuwa ishara ya mkuu wa mwanamke? Huku si kukufuru? Yesu ni mwanamume ambaye hajapotoshwa. Yeye ni Mungu; Yeye ni Kristo; Yeye ni Bwana. Anawezaje kuwa mwanamume kama Adamu ambaye alipotoshwa? Yesu ni mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu aliye mtakatifu sana. Unawezaje kusema kuwa Yeye ni Mungu aliye na uanaume wa Adamu? Kama ni hivyo, kazi yote ya Mungu haingekuwa si sahihi? Je, Yehova angeweza kuuweka ndani ya Yesu uanaume wa Adamu ambaye alidanganywa na yule nyoka? Je, si kupata mwili kwa wakati huu ni tukio jingine la kazi ya Mungu mwenye mwili ambaye ni tofauti kijinsia na Yesu lakini aliye kama Yeye katika asili? Bado unathubutu kusema kwamba Mungu mwenye mwili hawezi kuwa mwanamke kwa kuwa mwanamke ndiye aliyedanganywa kwanza na yule nyoka? Bado unathubutu kusema kwamba, kwa kuwa mwanamke ndiye mwenye najisi sana na ni chanzo cha upotovu wa wanadamu, Mungu hawezi kabisa kupata mwili kama mwanamke? Bado unathubutu kuendelea kusema kwamba “mwanamke siku zote atamtii mwanamume na hawezi kamwe kudhihirisha au kumwakilisha Mungu moja kwa moja”? Hukuelewa hapo nyuma; lakini sasa bado unaweza kuendelea kukufuru kazi ya Mungu, hususan mwili wa nyama wa Mungu? Kama huwezi kuona hili kwa uwazi kabisa, ni vizuri zaidi ukawa makini na ulimi wako, la sivyo upumbavu na ujinga wako ufichuliwe na ubaya wako uwekwe wazi. Usidhani kwamba unaelewa kila kitu. Nakueleza kwamba yote uliyokwishayaona na kuyapitia hayakutoshelezi wewe kuelewa hata sehemu ndogo kabisa ya mpango Wangu wa usimamizi. Hivyo kwa nini basi unakuwa mwenye kiburi sana? Talanta ndogo hiyo uliyonayo na maarifa kidogo hayo uliyonayo hayatoshelezi kutumika na Yesu hata katika sekunde moja ya kazi Yake! Je, una uzoefu kiasi gani hasa? Yale uliyoyaona na yote uliyoyasikia katika maisha yako yote na yale uliyoyafikiria ni kidogo kuliko kazi Ninayoifanya kwa muda mfupi sana! Ni bora usichambue na kutafuta kosa. Haijalishi una kiburi kiasi gani, wewe bado ni kuimbe tu mdogo kuliko mchwa! Vyote vilivyomo katika tumbo lako ni vichache zaidi ya vile vilivyomo katika tumbo la mchwa! Usifikiri kwamba kwa kuwa tu umepata uzoefu na ukubwa kiasi, unaweza kuashiria kwa shauku na kuzungumza kwa majivuno. Je, uzoefu wako na ukubwa wako sio matokeo ya maneno Niliyoyazungumza? Je, unaamini kwamba umeyanunua kupitia kufanya kwako kazi kwa bidii na kutokwa jasho? Siku hii, unaona kuwa nimepata mwili, na kwa sababu ya hili pekee unajawa na dhana nyingi hizo, na kutoka kwalo unakuwa na fikira nyingi isiyohesabika. Isingekuwa kwa kupata mwili Kwangu, bila kujali talanta ulizo nazo ni za ajabu kiasi gani, usingekuwa na dhana hizi nyingi; na. Si fikira zako zinatoka hapa? Kama si kupata mwili kwa Yesu mara hiyo ya kwanza, je, hata ungejua kuhusu kupata mwili? Je, si kwa sababu ya maarifa yako kutoka kwa kupata mwili mara ya kwanza ndio una ufidhuli kuthubutu kuhukumu kupata mwili kwa mara ya pili? Kwa nini ukuchunguze badala ya kuwa mfuasi mtiifu? Wakati umeingia katika mkondo huu na kuja mbele ya Mungu mwenye mwili, je, Angekuruhusu kuchunguza hili? Ni sawa kwako kuchunguza historia ya familia yako, lakini ukijaribu kuchunguza “historia ya familia” ya Mungu, inawezekanaje Mungu wa leo akuruhusu kufanya uchunguzi kama huo? Je, wewe si kipofu? Je, hujiletei dharau kwako mwenyewe?
Ikiwa tu kazi ya Yesu ingefanywa bila kukamilishwa na kazi katika hatua hii ya siku za mwisho, basi mwanadamu milele angeshikilia fikira kwamba Yesu tu ndiye Mwana wa pekee wa Mungu, yaani, Mungu ana mwana mmoja tu, na kwamba yeyote anayekuja baada yake akiwa na jina jingine hawezi kuwa Mwana pekee wa Mungu, sembuse Mungu Mwenyewe. Mwanadamu ana fikira kwamba yeyote ambaye anajitoa sadaka kwa ajili ya dhambi au yule ambaye anachukua mamlaka kwa niaba ya Mungu na anayewakomboa wanadamu wote ni Mwana wa Mungu wa pekee. Kuna baadhi ambao wanaamini kwamba alimradi Yeye anayekuja ni mwanamume, Anaweza kuchukuliwa kuwa ni Mwana wa Mungu wa pekee na mwakilishi wa Mungu, na hata kuna wale wanaosema kwamba Yesu ni Mwana wa Yehova, Mwana Wake wa pekee. Je, hii kweli siyo tu fikira iliyopita kiasi ya mwanadamu? Ikiwa hatua hii ya kazi haingefanywa katika enzi ya mwisho, basi wanadamu wote wangekuwa gizani sana kumhusu Mungu. Ingekuwa ni hivyo, mwanamume angejidhania kuwa ni wa juu sana kuliko mwanamke, na wanawake hawangeweza kamwe kuinua vichwa vyao juu na hivyo, hakuna mwanamke angeweza kuokolewa. Watu siku zote wanaamini kwamba Mungu ni mwanamume, na aidha kwamba siku zote Amemchukia mwanamke na asingempa wokovu. Ingekuwa ni hivyo, isingekuwa ukweli kwamba wanawake wote walioumbwa na Yehova na pia ambao wamepotoshwa, wasingeweza kuwa na fursa ya kuokolewa? Je, basi isingekuwa bure kwa Yehova kumuumba mwanamke, yaani, kumuumba Hawa? Na je, mwanamke asingeangamia milele? Kwa hiyo, hatua ya kazi katika siku za mwisho inafanywa ili kuwaokoa wanadamu wote, sio mwanamke tu Ikiwa kunaye anayefikiria kwamba ikiwa Mungu angepata mwili kama kike, ingekuwa kwa ajili ya kumwokoa mwanamke pekee, basi mtu huyo bila shaka angekuwa mpumbavu!
Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita. Kazi ya hatua hii inafanywa kwa msingi wa kazi ya Enzi ya Neema. Ikiwa hatua hizi mbili za kazi hazikuhusiana, kwa nini basi kusulubiwa hakurudiwi katika hatua hii? Kwa nini Sibebi dhambi za mwanadamu? Siji kupitia kuzaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu katika hatua hii, na wala Sibebi dhambi za wanadamu kupitia kusulubiwa; badala yake, Nipo hapa kumwadibu mwanadamu moja kwa moja. Ikiwa Mimi kumwadibu mwanadamu na kuja Kwangu si kwa njia ya Roho Mtakatifu na hakukufuata kusulubiwa, basi Nisingekuwa na sifa zinazostahili kumwadibu mwanadamu. Ni hasa kwa sababu Mimi ni mmoja na Yesu ndio Nakuja moja kwa moja kumwadibu na kumhukumu mwanadamu. Kazi katika hatua inajenga kabisa juu ya kazi katika hatua iliyotangulia. Hiyo ndiyo maana ni kazi kama hii tu ndiyo inaweza kumleta mwanadamu katika wokovu hatua kwa hatua. Yesu pamoja na Mimi tunatoka kwa Roho Mmoja. Ingawa miili Yetu haina uhusiano, Roho Zetu ni moja; ingawa kile Tunachofanya na kazi Tulizonazo hazifanani, kwa asili Tunafanana. Miili Yetu ina maumbo tofauti, lakini hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya enzi na mahitaji tofauti ya kazi Yetu; huduma Zetu hazifanani, hivyo kazi Tunayoileta na tabia Tunayoifichua kwa mwanadamu pia ni tofauti. Ndiyo maana kile ambacho mwanadamu anakiona na kukielewa leo hii si kama kile cha wakati uliopita; ni hivyo kwa sababu ya mabadiliko ya enzi. Ingawa jinsia na maumbo ya miili Yao ni tofauti, na kwamba hawakuzaliwa katika familia moja, sembuse katika kipindi kimoja, hata hivyo Roho Zao ni moja. Ingawa miili Yao haina uhusiano wa damu au kimwili kwa namna yoyote ile, haipingiki kwamba Wao ni Mungu kupata mwili katika vipindi viwili tofauti vya nyakati. Ni ukweli usiopingika kwamba Wao ni miili ya nyama ya Mungu, ingawa hawatoki katika ukoo mmoja na hawatumii lugha moja ya binadamu (mmoja alikuwa mwanamume aliyezungumza lugha ya Wayahudi na mwingine ni mwanamke anayezungumza Kichina pekee). Ni kwa sababu hizi ndiyo Wameishi katika nchi tofauti kufanya kazi ambayo inampasa kila mmoja kufanya, na katika nyakati tofauti vilevile. Licha ya ukweli kwamba Wao ni Roho moja, wakiwa na asili inayofanana, hakuna mfanano wa wazi kabisa kati ya ngozi za nje za miili Yao. Wanashiriki tu ubinadamu sawa, lakini sura ya nje ya miili Yao na kuzaliwa Kwao hakufanani. Mambo haya hayana athari katika kazi Zao au maarifa aliyonayo mwanadamu juu Yao, maana, kimsingi, Wao ni Roho moja na hakuna anayeweza kuwatenganisha. Ingawa Hawana uhusiano wa damu, nafsi Zao zote zinaongoza Roho Zao, ambazo zinawapa kazi tofauti katika nyakati tofauti. Miili Yao ilitoka kwa ukoo tofauti, kama namna ambavyo Roho wa Yehova si baba wa Roho wa Yesu na Roho wa Yesu si mwana wa Roho wa Yehova: Ni Roho moja. Vile vile, Mungu mwenye mwili wa leo hana uhusiano na Yesu kwa damu, na ilhali ni Wamoja; hii ni kwa sababu Roho Zao ni moja. Mungu anaweza kufanya kazi ya rehema na wema, vilevile na ile kazi ya hukumu ya haki na kumwadibu mwanadamu, na ile ya kuleta laana kwa mwanadamu; na hatimaye, Anaweza kufanya kazi ya kuuharibu ulimwengu na kuwaadhibu waovu. Je, hafanyi haya yote Mwenyewe? Je, hii si kudura ya Mungu? Aliweza kutangaza sheria kwa ajili ya mwanadamu na kumpa amri, na aliweza pia kuwaongoza Waisraeli wa awali katika kuishi maisha yao duniani na kuwaongoza kujenga hekalu na madhabahu, Akiwatawala Waisraeli wote. Kwa kutegemea mamlaka Yake, Aliishi pamoja na Waisraeli duniani kwa miaka elfu mbili. Waisraeli hawakuthubutu kumwasi; wote walimheshimu Yehova na walifuata amri Zake. Hii ilikuwa Kazi iliyofanywa kwa kutegemea mamlaka Yake na kudura Yake. Kisha, katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo kwa mwanadamu, maana Alikuwa amekuja kuwakomboa wanadamu kutoka dhambini. Aliweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo kusulubiwa Kwake kuliwakomboa wanadamu kutoka dhambini kabisa. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu kwa rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba ziweze kusamehewa milele. Alikuwa mwenye rehema, mwenye huruma, mwenye upendo na mstahimilivu. Na wale wote waliomfuata Yesu katika Enzi ya Neema nao pia walitafuta kuwa wastahimilivu na wenye upendo katika mambo yote. Walistahimili mateso kwa muda mrefu, na hawakuwahi kulipiza kisasi hata walipopigwa, kulaaniwa au kupigwa mawe. Lakini haya hayawezi kuwa hivyo tena katika hatua ya mwisho. Vivyo hivyo, hata ingawa Roho Zao zilikuwa moja, kazi ya Yesu na Yehova hazikufanana kabisa. Kazi ya Yehova haikuwa kwa ajili ya kukamilisha enzi bali kuiongoza, kukaribisha maisha ya wanadamu duniani. Hata hivyo, kazi sasa ni kuwashinda wale walio katika mataifa yasiyo ya Wayahudi na ambao wamepotoshwa sana, kuongoza sio tu familia ya China bali ulimwengu mzima. Inaweza kuonekana kwako kwamba kazi hii inafanywa Uchina pekee, lakini kwa kweli imekwishaanza kusambaa katika nchi za ughaibuni. Ni kwa nini wageni mara kwa mara wanatafuta njia ya kweli? Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi, na maneno yanayonenwa sasa yanaelekezwa kwa watu ulimwenguni kote. Na hili, nusu ya kazi tayari inafanywa. Kutoka kuumbwa kwa dunia hadi sasa, Roho wa Mungu ameendeleza hii kazi kubwa, na aidha Amefanya kazi tofauti katika enzi tofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya. Yeye ni Mungu, aliye mwingi wa rehema na wema; Yeye ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu na mchungaji wa mwanadamu; lakini pia Yeye ni hukumu, kuadibu, na laana kwa mwanadamu. Angeweza kumwongoza mwanadamu kuishi duniani kwa miaka elfu mbili na pia Angeweza kuwaokoa wanadamu waliopotoka kutoka dhambi. Leo, pia Anaweza kuwashinda wanadamu ambao hawamjui na kuwafanya wawe chini ya miliki Yake, ili kwamba wote wajinyenyekeze kwake kikamilifu. Mwishowe, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo ni dhalimu ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, ili kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, na upendo tu, si Mungu wa hekima, na maajabu tu, si Mungu mtakatifu tu, bali, hata zaidi ni Mungu anayemhukumu mwanadamu. Kwa waovu miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwenye kuchoma, kuhukumu na kuadhibu; kwa wale ambao wanapaswa kukamilishwa, Yeye ni mateso, usafishaji, na majaribu, na vilevile faraja, ruzuku, utoaji wa maneno, kushughulika na kupogoa. Na kwa wale ambao wanaondolewa, Yeye ni adhabu na vilevile malipo. Niambie, je, Mungu si mwenye enzi? Anaweza kufanya kazi yoyote na yote, sio tu kusulubiwa kama ulivyokuwa ukifikiri. Unamfikiria Mungu kuwa ni wa chini sana! Je, unaamini kwamba chote Anachoweza kufanya ni kukomboa wanadamu wote kupitia kusulubiwa kwako pekee? Na baada ya hilo, utamfuata mbinguni kula tunda kutoka mti wa uzima na kunywa kutoka mto wa uzima? ... Je, inaweza kuwa rahisi hivyo? Niambie, umekamilisha nini? Je, una uzima wa Yesu? Ni kweli ulikombolewa naye, lakini kusulubiwa kulikuwa ni kazi ya Yesu Mwenyewe. Ni wajibu gani umeukamilisha kama mwanadamu? Una uchaji Mungu wa nje pekee lakini huielewi njia Yake. Hivyo ndivyo unavyomdhihirisha? Ikiwa hujapata maisha ya Mungu au kuona tabia Yake yote ya haki, basi huwezi kudai kuwa mtu aliye na uzima, na hustahili kupitia katika lango la ufalme wa mbinguni.
Mungu si Roho pekee, Anaweza pia kuwa mwili: aidha, Yeye ni mwili wa utukufu. Yesu, ingawa hamjamwona, alishuhudiwa na Waisraeli, yaani, Wayahudi wa wakati huo. Mwanzoni alikuwa mwili wa nyama, lakini baada ya kusulubiwa, Aligeuka mwili wa utukufu. Yeye ni Roho anayezunguka mambo yote na Anaweza kufanya kazi katika kila mahali. Anaweza kuwa Yehova, au Yesu au Masihi; hatimaye, Anaweza pia kuwa Mwenyezi Mungu. Yeye ni haki, hukumu, na kuadibu; Yeye ni laana na ghadhabu, lakini pia Yeye ni rehema na wema. Kazi zote ambazo Amezifanya zinaweza kumwakilisha. Unasema Yeye ni Mungu ni wa aina gani? Hutaweza kuelezea kabisa. Yote unayoweza kusema ni: “Kuhusu Mungu ni wa aina gani, siwezi kuelezea.” Usihitimishe kwamba Mungu milele ni Mungu wa rehema na wema, kwa sababu tu Yeye alifanya kazi ya ukombozi katika hatua moja. Je, unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Mungu wa rehema na upendo pekee? Ikiwa Yeye ni Mungu wa rehema na mwenye upendo, kwa nini Ataikomesha enzi katika siku za mwisho? Kwa nini Ataleta chini majanga mengi sana? Ikiwa ni kama unavyofikiri, kwamba Yeye ni Mungu wa rehema na upendo kwa mwanadamu hadi mwisho kabisa, hata hadi katika enzi ya mwisho, basi kwa nini atatuma chini majanga kutoka mbinguni? Ikiwa Anampenda mwanadamu kama Anavyojipenda na kama Anavyompenda Mwanawe wa pekee, basi kwa nini Atatuma chini mapigo na mvua ya mawe kutoka mbinguni? Kwa nini Anamruhusu mwanadamu kuteseka na njaa na ndwele ya kufisha? Kwa nini anamruhusu mwanadamu kuteseka majanga haya? Hakuna yeyote kati wenu anayethubutu kusema Yeye ni Mungu wa aina gani, na hakuna anayeweza kuelezea. Je, unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Roho? Je, unathubutu kusema kuwa Yeye ni mwili wa Yesu pekee? Na unathubutu kusema kuwa Yeye ni Mungu ambaye milele atasulubiwa kwa ajili ya mwanadamu?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 16 Septemba 2018

Filamu za Kikristo "Wokovu" | Does Forgiveness of Sins Mean Full Salvation?

Filamu za Kikristo "Wokovu" | Does Forgiveness of Sins Mean Full Salvation?

Wokovu ni nini? Wale wanaoamini katika Bwana Yesu hufikiria kwamba ikiwa wataomba kwa dhati kwa Bwana, waungame dhambi zao, na kutubu, dhambi zao zitasamehewa, na watapewa wokovu, na Bwana Atakapokuja, wao watainuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni. Lakini je, wokovu kweli ni rahisi hivyo?
Shujaa katika filamu, Xu Zhiqian, ameamini katika Mungu kwa miaka mingi, akijitolea kwa shauku kwa Mungu, na kuacha kila kitu ili kutenda wajibu wake. Kwa ajili ya hili, alikamatwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China. Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, aliendelea kutekeleza wajibu wake, alipata uzoefu kidogo wa vitendo, na mahubiri yake na kazi ilitatua matatizo ya matendo kwa ndugu zake. Baadaye, mkewe pia alikamatwa, lakini hakulalamika, kuwa hasi, au kusambaratika.... Yote haya yalimshindia pongezi na sifa kutoka kwa ndugu zake. Xu Zhiqian anaamini kwamba ana uhalisi wa ukweli na kwamba hakuna tatizo kuingia katika ufalme wa mbinguni. Lakini punde tu, jaribio lisilotarajiwa lilimjia—mkewe anakufa chini ya mateso ya polisi wa CCP. Xu Zhiqian, akiwa na wasiwasi, ana dhana, kutoelewana, na malalamishi kuhusu Mungu, vilevile mawazo ya maasi dhidi ya na usaliti kwa Mungu.... Baadaye, wakati anapogundua anamsaliti Mungu, anaanza kutafakari, na kustaajabu kama watu ambao, kama yeye, hupitia majaribio na kisha kulalamika, hukosa kumwelewa Mugu, na humsaliti Mungu hakika huokolewa. Je, wao kweli wanastahili kuingia katika ufalme wa Mungu?
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Jumamosi, 15 Septemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro

Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye?

Ijumaa, 14 Septemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu,

Alhamisi, 13 Septemba 2018

Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Majadiliano Kuhusu Wokovu na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni

Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Majadiliano Kuhusu Wokovu na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni

Hasa ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni? Baadhi ya watu hufikiria dhambi zetu zinasamehewa pindi tunaposadiki Bwana, kwamba pindi tunapookolewa basi tunaokolewa milele, na kwamba mtu aina hii anaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni. Kisha kuna wale wanaosadiki kwamba, ingawa dhambi zetu zinasamehewa pindi tunaposadiki Bwana, bado tunafanya dhambi mara kwa mara na hatujafikia utakatifu, na kwa sababu Biblia inasema kwamba wale ambao si watakatifu hawawezi kumwona Bwana, basi ni vipi tunaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni wakati hatujafikia utakatifu? Hivyo ni nani aliye sahihi na nani asiye sahihi kutokana na mitazamo hii miwili? Tafadhali tazama pande zote mbili zikishiriki katika majadiliano makali!
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maandiko ya Biblia

Jumatano, 12 Septemba 2018

Swahili Praise and Worship Song "Ushuhuda wa Maisha" | Overcomers' Testimonies

Swahili Praise and Worship Song "Ushuhuda wa Maisha" | Overcomers' Testimonies

Siku moja huenda nikakamatwa na kuteswa na CCP, kuteseka huku ni kwa ajili ya haki, ambayo najua moyoni mwangu. Maisha yangu yakitoweka mara moja ghafla bin vu, bado nitasema kwa fahari kwamba nimemkubali Kristo wa siku za mwisho. Ikiwa siwezi kuona tukio kuu la ukuaji wa injili ya ufalme, bado nitatoa matarajio mazuri zaidi. Ikiwa siwezi kuiona siku ambayo ufalme unafanikishwa, lakini naweza kumwaibisha Shetani leo, basi moyo wangu utajawa na furaha na amani. Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani, mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu. Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki. Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia. Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.
Nikiwa mfia dini, na nisiweze tena kumtolea Mungu ushuhuda, injili ya ufalme bado itaenezwa kama moto wa nyikani na waumini wasiohesabika. Ingawa sijui naweza kuitembea njia hii yenye mabonde kwa umbali gani, bado nitautoa moyo wangu unaompenda Mungu. Nikiishuhudia kazi Yake ya siku za mwisho, nikitenda mapenzi Yake duniani, ni furaha yetu kujitoa wenyewe kueneza ukweli. Bila kutatizwa na dhiki, kama dhahabu safi iliyotengeneza katika tanuu, kutoka kwa ushawishi wa Shetani kunaibuka kikundi cha askari washindi. Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani, mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu. Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki. Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia. Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.
Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani, mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu. Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki. Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia. Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.
Maneno ya Mungu yanaenea kote duniani, mwanga umeonekana miongoni mwa binadamu. Ufalme wa Kristo unainuka na unaanzishwa ndani ya dhiki. Giza liko karibu kupita, alfajiri ya haki imewadia. Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda. Wakati na uhalisi umemtolea Mungu ushuhuda.
kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Imba Nyimbo Mpya

Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wimbo wa ibada

Jumanne, 11 Septemba 2018

Wimbo za Injili "Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu" | The Love of God Is the Truest Love

Wimbo za Injili "Ni Muumba Pekee Anayemhurumia Binadamu Huyu" | The Love of God Is the Truest Love

Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima, na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya; Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote. Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya: Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu. Ninawaangalia; Ninawasubiri; Niko kando yao….
Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa. Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu huruma na huba. Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu. Vilevile, Muumba pekee ndiye anayeweza kumpa huruma mwanadamu huyu na kufurahia viumbe vyake vyote. Moyo wake waruka na kuumia kwa kila matendo ya mwanadamu: Ameghadhibishwa, dhikishwa, na kuhuzunishwa juu ya maovu na kupotoka kwa binadamu; Ameshukuru, amefurahia, amekuwa mwenye kusamehe na mwenye kushangilia kutokana na kutubu na kuamini kwa binadamu; kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake vyote vipo juu ya na vinazungukia mwanadamu; kile Alicho na anacho vyote vinaonyeshwa kwa uzima au kwa minajili ya mwanadamu; uzima wa hisia Zake vyote vimeingiliana na uwepo wa mwanadamu.
Kwa minajili ya mwanadamu, Anasafiri na kuzungukazunguka; kwa utaratibu Anatoa kila sehemu ya maisha Yake; Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake…. Hajawahi kujua namna ya kuyahurumia maisha Yake, ilhali siku zote Amehurumia na kufurahia mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe aliumba…. Anatoa kila kitu Alichonacho kwa ubinadamu huu…. Yeye anatoa huruma na uvumilivu Wake bila masharti na bila matarajio ya kufidiwa. Anafanya hivi tu ili mwanadamu aweze kuendelea kuwepo mbele ya macho Yake, kupokea toleo Lake la maisha; Anafanya hivi tu ili mwanadamu siku moja aweze kunyenyekea mbele Yake na kutambua kwamba Yeye ni yule anayetosheleza kuwepo kwa binadamu na kuruzuku maisha ya viumbe vyote. Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa. Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu huruma na huba. Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu, huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, nyimbo za injili

Jumatatu, 10 Septemba 2018

Filamu za Kikristo 2018 | "Kumbukumbu Chungu" | Welcoming the Return of the Lord in Judgement

Filamu za Kikristo 2018 | "Kumbukumbu Chungu" | Welcoming the Return of the Lord in Judgement

Fan Guoyi alikuwa mzee wa kanisa la nyumba kule Uchina. Wakati wa zaidi ya miaka ishirini ya huduma, siku zote alimwiga Paulo, na kufanya kazi kwa bidii na akamtumikia Bwana kwa shauku kubwa. Aidha, alisadiki kabisa kwamba katika kufuata imani yake kwa njia hii, alikuwa akitenda mapenzi ya Baba wa mbinguni, na kwamba wakati Bwana angerudi, angenyakuliwa kwa hakika na kuenda kwenye ufalme wa mbinguni. Hata hivyo, wakati wokovu wa Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho ulipomjia, alishikilia kwa dhana zake. Alikataa, akapinga, na kushutumu kazi ya Bwana ya siku za mwisho tena na tena…. Baadaye, baada ya kufanya majadiliano kadhaa na wahubiri kutoka kwenye Kanisa la Mwenyezi Mungu, Fan Guoyi hatimaye alizinduliwa kwa ukweli, alielewa kwa kweli maana ya kutekeleza mapenzi ya Baba wa mbinguni, pamoja na jinsi ya kufuata imani yake kwa njia ambayo ingemwezesha kufikia wokovu na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni…. Kila mara anapokumbuka kile alichokuwa zamani, kumbukumbu hizo huchoma moyo wake kama miiba …
Soma zaidi: Umeme wa Mashariki Video.

Jumapili, 9 Septemba 2018

Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?"

Matamshi ya Roho Mtakatifu | "Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?"

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyoongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa kwa binadamu, na tofauti kwamba mmoja anachukuliwa katika mimba na Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki. Mmoja ni Mwanzo na mwingine Mwisho. Mmoja ni mwili usio na dhambi na mwingine ni mwili unaokamilisha ukombozi, Anaendelea na kazi hiyo na kamwe hana dhambi hata. Wote ni Roho mmoja lakini wanaishi katika miili tofauti na walizaliwa katika sehemu tofauti. Na wametenganishwa na maelfu kadhaa ya miaka. Ilhali kazi Zao ni kijalizo kwa nyingine, hazina mgongano kamwe na zinaweza kuzungumziwa kwa wakati mmoja. Wote ni watu, lakini mmoja ni mtoto wa kiume na mwingine mtoto mchanga wa kike."
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kuonekana kwa Mungu

Jumamosi, 8 Septemba 2018

Maonyesho ya Mungu | "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe"

Maonyesho ya Mungu | "Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe"

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu hasa wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Ukiweza kuliona hili wazi, utaweza kuhusisha sehemu zote za Mungu, na utaacha kuthamini sana kazi Yake ya uungu, na kuwa mwenye kupuuza sana kazi Yake katika ubinadamu, na hautazidi mipaka wala kupita njia za michepuo. Kwa jumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika."
Sikiliza zaidi:  Umeme wa Mashariki video
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maneno ya Mungu

Ijumaa, 7 Septemba 2018

Maneno ya Mungu | "Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini" | Can Your Faith Gain the Praise of God?

Maneno ya Mungu | "Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini" | Can Your Faith Gain the Praise of God?

Mwenyezi Mungu alivyosema, "Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, haya ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Kutenda kama huku pekee ndiko hutosheleza Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli."
Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, maneno ya Mungu

Alhamisi, 6 Septemba 2018

Swahili Christian Sketch "Onyo Kutoka kwa Historia" (Kichekesho)

Swahili Christian Sketch "Onyo Kutoka kwa Historia" (Kichekesho)

Miaka elfu mbili iliyopita, wakati Bwana Yesu alipotokea na kufanya kazi, Mafarisayo walikwamia sheria na kukashifu kazi Yake, wakisema kuwa kazi Yake ilienda zaidi ya Maandiko.Ili kulinda hali zao na maisha yao, walijitahidi kwa nguvu zao zote ili kuwazuia watu kutafuta kazi ya Bwana Yesu, na kujiunga na serikali ya Kirumi kumsulubisha msalabani. Katika siku za mwisho, wakati Bwana Yesu anapoonekana tena katika mwili ili kufanya kazi, viongozi wa ulimwengu wa kidini wanarudia tukio la janga la kihistoria la upinzani wa Mafarisayo kwa Bwana Yesu. Je, wanapingaaje kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Kupitia kwa mchungaji anayeigiza kama Mfarisayo katika tukio, mchezo huu unadhihirisha jinsi wachungaji na wazee wa kisasa wanavyoshikilia Biblia ili kumpinga Mungu, na inaonyesha wazi kwamba njia wanayoitembea ni sawa na ile ya Mafarisayo.
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumjua Mungu,