Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana|”Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu”

Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli. Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | “Sauti ya Moyo ya Kiumbe Aliyeumbwa” (Video za Kikristo)

Mungu wa vitendo na wa kweli, upendo ndani ya moyo wangu. Mimi ni vumbi lakini ninaweza kuona uso Wako. Ninawezaje kukosa kukuabudu?

Mungu ndiye Mwanzo na tena Mwisho | Kwaya ya Injili

Mungu ndiye Mwanzo (Mungu ndiye Mwanzo) na Mwisho (na Mwisho); ni Yeye Mwenyewe Anayetekeleza kazi Yake na hivyo lazima iwe Yeye Mwenyewe Anayemaliza enzi ya kale. Huo ndio ushahidi kuwa Yeye humshinda Shetani (humshinda Shetani) na huishinda dunia, ushahidi kuwa Yeye huishinda dunia.

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki

Nitakupa Wewe upendo wa kweli, na sitakuacha Usubiri. Mimi nitakupa Wewe upendo safi, na tafadhali furahia upendo wangu. Nitakupa Wewe upendo wangu wote, na kukuacha upate upendo wangu. Nitakupenda Wewe kwa wakati wote; kukuridhisha Wewe ni matamanio yangu.

Jumanne, 11 Desemba 2018

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu"

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Tabia ya mwanadamu lazima ibadilishwe kuanzia maarifa ya dutu yake na kupitia mabadiliko katika mawazo yake, asili, na mtazamo wa akili—kwa njia ya mabadiliko ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndio mabadiliko ya kweli yatapatikana katika tabia ya mwanadamu. Tabia ya upotovu ya mwanadamu inatokana na hali yake ya kupewa sumu na kukanyagwa na Shetani, kutokana na madhara mabaya sana ambayo Shetani ameweka katika mawazo yake, maadili, ufahamu, na hisia. Ni hasa kwa sababu mambo haya ya msingi ya mwanadamu yamepotoshwa na Shetani, na ni tofauti kabisa na jinsi Mungu aliwaumba kwa asili,kwamba mwanadamu humpinga Mungu na haelewi ukweli. Hivyo, mabadiliko katika tabia za mwanadamu lazima yaanze na mabadiliko katika mawazo yake, ufahamu na hisia ambayo yatabadilisha maarifa yake ya Mungu na maarifa yake ya ukweli."

Jumatatu, 10 Desemba 2018

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)

Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habalidiliki na humfafanua kulingana na Bibilia, kana kwamba mwanadamu ameona ndani ya usimamizi wa Mungu, kana kwamba kila kitu Atendacho Mungu kiko mikononi mwa mwanadamu. Wanadamu ni wa kufanya mzaha pakubwa, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha lugha ya kushawishi ya kujivuna. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, Bado Nasema kwamba bado humfahamu Mungu, kwamba hakuna walio wapinzani wa Mungu zaidi, na kwamba unamshutumu Mungu, kwa kuwa huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili ya Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hajui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi na kwa sababu badala ya kufuata ukweli, maarifa yake yote ya Mungu yametolewa kutoka kwenye chanzo kimoja, chenye ugumu na kisichobadilika. Hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Amesulubishwa kwa mara nyingine msalabani na mwanadamu. ... Je wewe ni mmoja wa wale ambao wamemsulubisha Yesu msalabani tena? Mwisho, Ninasema hivi: Ole wao wamsulubishao Mungu."

Jumamosi, 8 Desemba 2018

Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hekima ya Mungu

Jinsi ya Kutafuta Nyayo za Mungu

I
Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, lazima tutafute mapenzi ya Mungu, tutafute maneno ya Mungu na matamshi ya Mungu, tutafute maneno ya Mungu na matamshi Yake. Kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, pana sauti ya Mungu, sauti Yake; palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu, matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu, pana sura, sura ya Mungu, na palipo na sura ya Mungu, pana ukweli, njia, na uzima.
II
Mkitafuta nyayo za Mungu, mlipuuza maneno kuwa, "Mungu ni ukweli, njia, na uzima." Hivyo watu wengi wapokeapo ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata kukosa kutambua kuonekana kwa Mungu. Ni kosa kubwa sana! Ni kosa kubwa sana! Kuonekana kwa Mungu hakuwezi kulingana na dhana za mwanadamu, sembuse Mungu kuonekana kwa ombi la mwanadamu. Anapofanya kazi Yake, Anafanya chaguo Lake, Anafanya chaguo Lake, anayo mipango Yake. Zaidi ya hayo, ana malengo Yake mwenyewe, na mbinu Zake, mbinu Zake mwenyewe. Anapofanya kazi Yake, hahitaji kujadili kazi Yake na mtu, kutafuta ushauri wa mtu, sembuse kumuarifu kila mtu. Hii ni tabia ya Mungu, inafaa kujulikana na wote.
III
Ukiwa na hamu kushuhudia kuonekana kwa Mungu, ukiwa tayari kutafuta nyayo za Mungu, basi kwanza lazima uvuke dhana zako mwenyewe. Sharti usimfanyie Mungu madai ya kufanya hili ama lile, wala hufai kumzuia, katika mipaka yako mwenyewe na kumwekea mipaka katika dhana zako mwenyewe. Badala yake, wafaa kuuliza jinsi ya kutafuta nyayo za Mungu, kukubali kuonekana kwa Mungu, na jinsi unavyopaswa kutii kazi mpya ya Mungu; ndilo linapaswa kufanywa na mtu, kufanywa na mwanadamu. Kwa kuwa hakuna, mwingine aliye ukweli, na hakuna aliye na, aliye na ukweli, mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii. Kwa kuwa hakuna aliye ukweli, hakuna aliye ukweli, na hakuna aliye na, aliye na ukweli, mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii. Mwanadamu anapaswa kutafuta, kukubali na kutii.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Ijumaa, 7 Desemba 2018

Wimbo Mpya wa Dini | "Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa" | Have You Followed God's Footsteps?

Wimbo Mpya wa Dini | "Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa" | Have You Followed God's Footsteps?

Kazi ya Mungu inaendelea kuwa bora; ingawa kusudi linabaki bila kubadilika, mbinu ya kazi Yake inabadilika daima, na hivyo pia wale wanaomfuata. Kadiri ambavyo Mungu anafanya kazi zaidi, ndivyo anavyozidi mwanadamu kumjua, kikamilifu, ndivyo tabia ya mwanadamu inavyozidi kubadilika pamoja na kazi Yake ifaavyo. Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa; Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima. Yeye kamwe harudii kazi ya zamani, kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.
Mungu hadumishi kazi ile ile; inabadilika kila mara na ni mpya daima. Ni sawa na Mungu kunena maneno mapya na kufanya kazi mpya kila siku kwako. Hii ni kazi ambayo Mungu anafanya; umuhimu upo katika "ajabu," na "mpya." "Mungu habadiliki na Yeye atakuwa Mungu daima." Huu ni msemo ambao hakika ni ukweli. Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa; Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima. Yeye kamwe harudii kazi ya zamani, kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.
Lakini kwa kuwa kazi ya Mungu hubadilika kila mara, kwa wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu, na wanadamu wapumbavu wasiojua ukweli, Wao huishia kuwa wapinzani wa Mungu. Kiini cha Mungu hakitabadilika kamwe; Mungu ni Mungu kila mara na kamwe sio Shetani. Lakini hii haimaanishi kuwa kazi Yake haibadiliki, na ipo daima kama kiini Chake. Unasema kuwa Mungu habadiliki kamwe, lakini utaeleza vipi "sio nzee kamwe, mpya daima"? Kazi ya Mungu inakua na kubadilika, Anaonyesha mapenzi Yake na kufanya yajulikane kwa mwanadamu pia. Kazi ya Mungu inaendelea kuboreshwa; Kazi Yake kamwe sio nzee na ni mpya daima. Yeye kamwe harudii kazi ya zamani, kazi ambayo haijafanywa awali tu ndiyo Atakayoifanya.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Sikiliza zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu video

Alhamisi, 6 Desemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Themanini na Sita

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Themanini na Sita

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia. Kwa wale Ninaowapenda, Nitawapenda daima mpaka mwisho kabisa na upendo hautabadilika kamwe. Kwa wale Ninaowachukia, moyo Wangu hauguswi hata kidogo bila kujali ni wazuri kiasi gani. Hii ni kwa sababu wao sio Wangu na hawana sifa Zangu na hawana uzima Wangu. Hiyo ni kusema, hawakuamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi, kwani Mimi siwezi kukosea. Hiyo ni kusema kwamba kila Ninachofanya kinaitwa kitakatifu na chenye heshima na Sina majuto yoyote kamwe. Katika macho ya watu, Mimi ni mkatili sana; lakini hujui kwamba Mimi ni Mungu Mwenyewe mwenye haki na uadhama? Kila kitu Changu ni sahihi; wale Ninaowachukia bila shaka watapata laana Zangu na wale Ninaowapenda kwa hakika watapokea baraka Zangu. Hii ni tabia Yangu takatifu na isiyokiukwa na hakuna mwanadamu atakayeibadilisha; hili ni bila shaka!
Leo, wale ambao kwa kweli wanakubaliana na nia Zangu hakika watakamilishwa na Mimi, kwa maana kazi Yangu ni wazi na kamilifu na Siachi chochote kisicho kamili; wale Ninaowalaani watachomwa. Hivyo kwa nini watu wengi wamelaaniwa na Mimi na bado Roho Mtakatifu bado anafanya kazi Yake juu yao (hili linasemwa kuhusiana na Mimi kutoishi katika hekalu chafu)? Je, mnaelewa maana halisi ya mambo yote na vitu vyote kuhusu kutoa huduma kwa Kristo? Roho Mtakatifu hufanya kazi Yake kupitia kwa wao Ninapotumia huduma yao, lakini kwa kawaida wakati hawako katika huduma Yangu kimsingi hawajapewa nuru katika roho yao. Hata wakinitafuta, ni kwa bidii, na hii ni hila ya Shetani, kwani kwa nyakati za kawaida, hawatilii maanani kazi Yangu hata kidogo na hawahurumii kabisa mizigo Yangu. Sasa wazaliwa Wangu wa kwanza wamekua, na hivyo Ninawafukuza na kwa hiyo Roho Wangu ameondoka kutoka kila mahali, na mkazo maalum unawekwa kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, unaelewa? Mambo yote yanabaki kwa matendo Yangu, yanabaki kwa majaaliwa Yangu, na kubaki kwa maneno yote kutoka kinywani Mwangu. Maeneo yote ambayo yamepokea baraka Zangu lazima yawe mahali ambapo Nafanya kazi, na pia mahali ambapo kazi Yangu inatekelezwa. China ni taifa ambapo Shetani anaabudiwa zaidi na hivyo Nimelilaani, na pia ni taifa ambalo limefanya mengi zaidi kunitesa. Mimi kabisa Sitafanya kazi Yangu kwa watu chini ya ushawishi wa joka kuu jekundu. Je, unaelewa maana halisi ya neno Langu? Hata hivyo, idadi za wana Wangu na watu Wangu ni chache. Hakika kila kitu ki mikononi Mwangu na nguvu yako inapaswa kulenga na juhudi zaidi inapaswa kutumiwa kwa wale ambao Nimewachagua na kuwaamulia kabla. Hiyo ni kusema, wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza wanapaswa kutenda haraka ili kubeba mizigo iliyo juu ya mabega Yangu mapema iwezekanavyo na kuweka jitihada zote katika kazi Yangu.
Wale wanaonitumikia, sikilizeni! Mnaweza kupokea baadhi ya neema Yangu wakati mnanitumikia. Yaani, ninyi mtajua kwa wakati kuhusu kazi Yangu ya baadaye na mambo ambayo yatatokea baadaye, lakini hamtafurahia hilo kabisa. Hii ni neema Yangu. Wakati huduma Yako imekamilika, ondoka mara moja na usikawie. Wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza hawapaswi kuwa wenye kiburi, lakini mnaweza kujivunia, kwa kuwa Nimewapa baraka za milele kwenu. Wale ambao ni walengwa wa uangamizaji hampaswi kujiletea shida au kuhisi huzuni kwa ajili ya hatima yenu; ni nani aliyekufanya kuwa mzawa wa Shetani? Baada ya kufanya huduma yako kwa ajili Yangu, unaweza kurudi tena kwenye shimo lisilo na mwisho kwa sababu hutakuwa tena na matumizi Kwangu na Nitaanza kuwashughulikia na kuadibu Kwangu. Mara Ninapoanza kazi Yangu huwa Sikomi kamwe; kile Ninachofanya kitatimizwa na kile Ninachotimiza kitadumu milele. Hili linatumika kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanangu, watu Wangu, na hili linawahusu ninyi pia—Mimi kuwaadibu ninyi kutakuwa kwa milele. Nimewaambia mara nyingi kabla: Waovu wanaonipinga hakika wataadibiwa na Mimi. Unaponipinga bila ukaripiaji kutoka kwa Roho Mtakatifu, tayari umelaaniwa na baada ya hapo utapigwa chini na mkono Wangu. Ukipokea nidhamu ya Roho Mtakatifu unapokuwa na mawazo mabaya kunihusu, basi umepokea baraka Yangu. Hata hivyo, lazima uwe mwangalifu daima, usiwe mzembe kamwe, na usiwe mvivu kamwe.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Jumatano, 5 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno."
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumanne, 4 Desemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati. Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi. Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. Kwa hivyo, miaka kadhaa baada ya Yeye kuondoka, Mathayo aliunda kizazi chake, na wengine pia walifanya kazi kubwa ambayo ilikuwa ya mapenzi ya mwanadamu. Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwa na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kujua. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kumaliza kazi ya Mungu? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kumalizia. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno ambayo Alikuwa Ameyasema pia yalikuwa yamefika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimya kimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko na makosa yake yote yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo. Kazi ya Yehova ilikuwa uumbaji wa ulimwengu, ilikuwa mwanzo; awamu hii ya kazi ni mwisho wa kazi, na ni hitimisho. Hapo mwanzo, kazi ya Mungu ilifanyika miongoni mwa wateule wa Israeli, na ilikiwa mapambazuko ya kipindi kipya katika pahali patakatifu zaidi ya popote. Awamu ya mwisho ya kazi inafanywa katika nchi ambayo ni chafu zaidi ya zote, kuhukumu ulimwengu na kuleta enzi kwenye kikomo. Katika awamu ya kwanza kazi ya Mungu ilifanyika katika maeneo yenye kung’aa kuliko maeneo yote, na awamu ya mwisho inafanyika katika maeneo yaliyo katika giza kuliko maeneo yote, na giza hili litaondolewa, na mwanga kufunguliwa, na watu wote kushindwa. Wakati watu wa maeneo haya yaliyo chafu kuliko yote na yaliyo na giza watakuwa wameshindwa na idadi yote ya watu wametambua kuwa Mungu yupo, na ya kuwa ni Mungu wa kweli, na kila mtu Amemwamini kabisa, basi ukweli huu utatumika kutekeleza kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima. Awamu hii ya kazi ni ya ishara: Punde tu kazi ya kipindi hiki itakapomalizika, kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi itafikia mwisho kabisa. Mara baada ya wale walioko katika maeneo yaliyo na giza kuliko yote watakapokuwa wameshindwa, bila shaka itakuwa hivyo pia kila mahali pengine. Kwa hivyo, kazi ya ushindi tu katika China inabeba ishara ya maana. China inajumuisha nguvu zote za giza, na watu wa China wanawakilisha wale wote ambao ni wa mwili, wa Shetani, na wa mwili na damu. Ni watu wa China ndio wamepotoshwa sana na joka kubwa jekundu, ambao wana upinzani wenye nguvu dhidi ya Mungu, ambao wana ubinadamu ulio mbovu zaidi na ulio mchafu, na kwa hivyo hao ni umbo asili la wanadamu wote wenye matendo maovu. Hii si kusema kwamba nchi nyingine hazina shida kabisa; dhana za mwanadamu ni sawa zote, na ingawa watu wa nchi hizi wanaweza kuwa na uhodari mzuri, ikiwa hawamjui Mungu, basi ni lazima iwe kwamba wanampinga. Kwa nini Wayahudi pia walimpinga na kumwasi Mungu? Kwa nini Mafarisayo pia walimpinga? Kwa nini Yuda alimsaliti Yesu? Wakati huo, wengi wa wanafunzi hawakumjua Yesu. Kwa nini, baada ya Yesu kusulubiwa na kufufuliwa tena, watu bado hawakumwamini? Je, uasi wa mwanadamu sio sawa wote? Ni tu kwamba watu wa China wamefanyika mfano, na watakaposhindwa watakuwa mfano na kielelezo, na watatumika kama kumbukumbu kwa wengine. Kwa nini mimi daima Nimesema yakuwa nyinyi ni kiungo cha mpango wangu wa usimamizi? Ni katika watu wa China ambapo upotovu, uchafu, udhalimu, upinzani, na uasi unadhihirishwa kikamilifu zaidi na kufichuliwa kwa hali zao mbalimbali. Kwa upande mmoja, wao ni wa kimo cha umaskini, na kwa upande mwingine, maisha yao na mawazo yao ni ya nyuma kimaendeleo, na tabia zao, mazingira ya kijamii, familia ya kuzaliwa—yote ni ya umaskini na ya nyuma kimaendeleo kuliko yote. Hadhi yao, pia, ni ya chini. Kazi katika eneo hili ni ya ishara, na baada ya kazi hii ya majaribio hufanywa kwa ukamilifu wake, na kazi yake inayofuata itakwenda vizuri zaidi. Kama awamu hii ya kazi inaweza kukamilika, basi kazi inayofuata itakamilika bila shaka. Mara baada ya awamu ya kazi hii kutimizwa, na mafanikio makubwa kufikiwa kikamilifu, kazi ya ushindi katika ulimwengu mzima itakua imefikia kikomo kamili. Kwa kweli, mara baada ya kazi miongoni mwenu imekuwa ya mafanikio, hii itakuwa sawa na mafanikio katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa sababu Yangu kuwafanya mfano wa kuigwa na kielelezo. Uasi, upinzani, uchafu, udhalimu—yote haya hupatikana kwa watu hawa, na ndani yao pamewakilishwa uasi wote wa wanadamu. Wao ni wa kushangaza kweli. Hivyo, wanafanywa kuwa mfano wa ushindi, na punde tu watakaposhindwa watakuwa kama ilivyo kawaida kielelezo na mfano wa kuigwa na wengine. Hakuna kilichokuwa cha ishara zaidi ya awamu ya kwanza iliyofanyika katika Israeli: Waisraeli walikuwa watakatifu sana na wenye upotovu wa chini zaidi kuliko watu wote, na hivyo pambazuko la kipindi kipya katika nchi hii kilibeba umuhimu mkubwa. Inaweza kusemwa kwamba mababu wa wanadamu walitoka Israeli, na kwamba Israeli, ilikuwa watani wa kazi ya Mungu. Hapo mwanzo, watu hawa walikuwa watakatifu sana, na wote walimwabudu Yehova, na kazi ya Mungu ndani yao iliweza kuzaa mazao makubwa. Biblia nzima inarekodi kazi ya enzi mbili: Moja ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria, na moja ilikuwa kazi ya Enzi ya Neema. Agano la Kale hurekodi maneno ya Yehova kwa Waisraeli na kazi Yake katika Israeli; Agano Jipya linarekodi kazi ya Yesu huko Uyahudi. Lakini kwa nini Biblia haina majina yoyote ya Kichina? Kwa sababu sehemu mbili za kwanza za kazi ya Mungu zilifanyika katika Israeli, kwa sababu watu wa Israeli walikuwa wateule—ambayo ni kusema kwamba wao walikuwa wa kwanza kukubali kazi ya Bwana. Walikuwa wenye upotovu wa chini zaidi ya wanadamu wote, na hapo mwanzo, walikuwa na nia ya kumtazamia Mungu na kumheshimu Yeye. Walitii maneno ya Bwana, na daima walitumika katika hekalu, na walivaa mavazi ya kikuhani au mataji. Walikuwa watu wa kwanza kabisa kuabudu Mungu, na chombo cha kwanza kabisa cha kazi yake. Watu hawa walikuwa kielelezo na mfano wa kuiga kwa wanadamu wote. Walikuwa kielelezo na mfano wa kuiga wa utakatifu na haki. Watu kama Ayubu, Ibrahim, Lutu, au Petro na Timotheo—wote walikuwa Waisraeli, na vielelezo na mifano mitakatifu zaidi ya watu wote. Israeli ilikuwa nchi ya kwanza ya kuabudu Mungu miongoni mwa wanadamu wote, na watu wengi wenye haki walitoka hapa kuliko mahali pengine popote. Mungu Alifanya kazi kati yao ili aweze kusimamia vizuri mwanadamu katika nchi zote na katika siku zijazo. Mafanikio yao na haki ya ibada yao ya Yehova yaliandikwa kwenye kumbukumbu, ili waweze kuhudumu kama vielelezo na mifano kwa watu waliokuwa nje ya Israeli wakati wa Enzi ya Neema; na matendo yao yamezingatia miaka elfu kadhaa ya kazi, mpaka hivi leo.
Baada ya kuanzishwa kwa dunia, hatua ya kwanza ya kazi ya Mungu ilifanyika katika Israeli, na hivyo Israeli palikuwa mahali pa kuzaliwa kwa kazi ya Mungu duniani, na msingi wa kazi ya Mungu duniani. Upeo wa kazi ya Yesu ulienea kote Uyahudi. Wakati wa kazi Yake, wachache sana wa wale waliokuwa nje ya Uyahudi walijua jambo hilo, kwa kuwa hakufanya kazi yoyote nje ya Uyahudi. Leo, kazi ya Mungu imeletwa nchini China, na inatekelezwa kabisa ndani ya eneo hili. Katika awamu hii, hakuna kazi inayozinduliwa nje ya China; kuenea kwake zaidi ya China ni kazi ambayo itakuja baadaye. Hatua hii ya kazi inafuatilia kutoka kwa hatua ya kazi ya Yesu. Yesu alifanya kazi ya ukombozi, na hatua hii ni kazi inayofuata; ukombozi umekamilika, na katika hatua hii hakuna haja ya kuzaliwa na Roho Mtakatifu, kwa sababu hatua hii ya kazi ni tofauti na hatua ya mwisho, na, zaidi ya hayo, kwa sababu China ni tofauti na Israeli. Hatua ya kazi iliyofanywa na Yesu ilikuwa kazi ya ukombozi. Mtu alimwona Yesu, na si muda mrefu baadaye, kazi Yake ilianza kuenea kwa Wayahudi. Leo, kuna wengi ambao wanaamini katika Mungu katika Amerika, Uingereza na Urusi, hivyo kwa nini kuna wachache nchini China? Kwa sababu China ni taifa lililotengwa zaidi. Kwa hivyo, China ilikuwa ya mwisho kukubali njia ya Mungu, na hata sasa imekuwa chini ya miaka mia tangu kuikubali—baadaye zaidi ya Amerika na Uingereza. Hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu inafanywa katika nchi ya China ili kutamatisha kazi Yake, na ili kazi Yake yote iweze kukamilika. Watu wa Israeli wote walimwita Yehova, Bwana wao. Wakati huo, walimwona kama kichwa cha familia zao, na Israeli yote ikawa familia kubwa ambapo kila mtu alimwabudu Bwana wao Yehova. Roho wa Bwana mara nyingi Aliwatokea, naye akanena na kutamka sauti Yake, na kutumia nguzo ya wingu na sauti kuongoza maisha yao. Wakati huo, Roho alitoa mwongozo Wake katika Israeli moja kwa moja, Akizungumza na kutoa sauti Yake kwa watu, na waliona mawingu na kusikia sauti za ngurumo, na kwa njia hii Aliyaongoza maisha yao kwa maelfu kadhaa ya miaka. Kwa hiyo, watu wa Israeli pekee wamekuwa wakimwabudu Yehova daima. Wanaamini kwamba Yehova ni Mungu wao, na si Mungu wa Mataifa. Hii haishangazi: Yehova, hata hivyo, alikuwa amefanya kazi kati yao kwa karibu miaka 4,000.Katika nchi ya China, baada ya kulala kwa maelfu ya miaka, sasa tu ndipo wapotovu wamejua kwamba mbingu na ardhi na vitu vyote hazikuundwa kwa kawaida, bali zilifanywa na Muumba. Kwa sababu injili hii imekuja kutoka nje ya nchi, hao wenye mawazo ya kikabaila, wapinga mageuzi wanaamini kwamba wote wanaokubali injili hii wanafanya uhalifu mkubwa, ni vijibwa wanaomsaliti Budha—babu wao. Zaidi ya hayo, wengi wa wenye mawazo haya ya kikabaila wanauliza, Watu wa China wanawezaje kuamini katika Mungu wa wageni? Je, hawawasaliti baba zao? Je, hawatendi mabaya? Leo, watu wamesahau kitambo kwamba Yehova ndiye Mungu wao[a]. Wamemsukuma Muumba nyuma ya akili zao kitambo, na badala yake wanaamini katika nadharia ya mageuko, ambayo ina maana kwamba mtu amebadilika kutoka kuwa sokwe, na kwamba ulimwengu wa asili umekuwapo daima. Chakula chochote nzuri kinachofurahiwa na wanadamu kinatolewa na ulimwengu, kuna utaratibu wa maisha na kifo cha mwanadamu, na hakuna Mungu anayetawala vyote. Zaidi ya hayo, kuna watu wengi wasioamini Mungu ambao wanasema kwamba kuamini katika utawala wa Mungu juu ya vitu vyote ni ushirikina. Lakini je, sayansi inaweza kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu? Je, sayansi inaweza kutawala juu ya wanadamu? Kuhubiri injili katika nchi kama hiyo sio kazi rahisi, na inahusisha vikwazo vingi. Leo, je, si kuna wengi ambao wanapinga Mungu kwa njia hii?
Watu wengi walifanya kazi ya Yesu kuwa mfano dhidi ya ile ya Bwana, na walipogundua kutofautiana, walimpigilia misumari Yesu msalabani. Lakini kwa nini kulikuwa na kutofautiana kati ya kazi yao? Ilikuwa, kwa sehemu, kwa sababu Yesu alifanya kazi mpya, na pia kwa sababu kabla ya Yesu kuanza kazi Yake, hakuna mtu aliyeandika ukoo Wake. Kama mtu angefanya hivyo, basi kusingekuwa na haja ya kuwa na wasiwasi, na nani bado angempigilia misumari Yesu msalabani? Ikiwa Mathayo angeandika ukoo wa Yesu miongo kadhaa kabla, basi Yesu asingepitia mateso hayo makuu. Je, si hivyo? Mara tu watu walipojifunza kuhusu uzao wa Yesu—kwamba alikuwa mwana wa Ibrahimu, na mzao wa Daudi—basi wangekoma kumtesa Yeye. Je, si jambo la kusikitisha kwamba uzazi Wake ulikawia mno kuandikwa? Na ni jambo la kusikitisha kwamba Biblia inarekodi tu hatua mbili za kazi ya Mungu: hatua moja ambayo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria, na moja ambayo ilikuwa kazi ya Enzi ya Neema; hatua moja ambayo ilikuwa kazi ya Bwana, na moja ambayo ilikuwa kazi ya Yesu. Ingekuwa bora zaidi kama nabii mkuu angetabiri kazi ya leo. Kungekuwa na sehemu ya ziada ya Biblia yenye mada "Kazi ya Siku za Mwisho"—je, si hiyo ingekuwa bora sana? Kwa nini mtu lazima apitie ugumu sana leo? Mlikuwa na wakati mgumu sana! Ikiwa mtu yeyote anastahili kuchukiwa, ni Isaya na Danieli kwa ajili ya kutotabiri kazi ya siku za mwisho, na kama mtu yeyote anastahili kulaumiwa, ni mitume wa Agano Jipya ambao hawakuandika orodha ya uzazi wa kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili mapema. Aibu iliyoje! Mnalazimika kutafuta ushahidi kila mahali, na hata baada ya kupata vipande kiasi vya maneno madogo bado hamwezi kujua kama kweli ni ushahidi. Aibu iliyoje! Kwa nini Mungu ni msiri sana katika kazi Yake? Leo, watu wengi bado hawajapata ushahidi thabiti, lakini pia hawawezi kukataa. Basi wanapaswa kufanya nini? Hawawezi kumfuata Mungu kwa uthabiti, wala pia hawawezi kuendelea mbele katika shaka hiyo. Na hivyo, "wasomi mahiri na wenye vipawa" wengi hukubali mtazamo wa "jaribu na kuona" wanapomfuata Mungu. Hii ni shida nyingi sana! Je, si mambo yangekuwa rahisi sana kama Mathayo, Mariko, Luka na Yohana wangeweza kutabiri yajayo? Ingekuwa bora kama Yohana angekuwa ameona ukweli wa ndani wa uzima katika ufalme—ni jambo la kusikitisha sana kwamba yeye aliona tu maono na hakuona kazi halisi, yakinifu duniani. Aibu iliyoje! Ni nini kibaya na Mungu? Kwa nini, baada ya kazi yake kwenda vizuri sana katika Israeli, sasa Amefika China, na kwa nini alipaswa kuwa mwili, na kufanya kazi na kuishi kati ya watu? Mungu hamfikirii mtu kabisa! Sio tu kwamba Hakuwaambia watu mapema, lakini pia ghafla Alileta adabu na hukumu Yake. Kwa kweli haileti maana! Mara ya kwanza Mungu kuwa mwili, Aliteseka dhiki nyingi kutokana na kutomwambia mwanadamu ukweli wote wa ndani mapema. Hakika Yeye Hawezi kuwa Amesahau hilo? Na kwa nini bado Hamwambii mtu wakati huu? Leo, ni bahati mbaya kwamba kuna vitabu sitini na sita tu katika Biblia. Kunahitaji tu kuwa na mmoja zaidi unaotabiri kazi ya siku za mwisho! Je, hufikiri? Hata Yehova, Isaya na Daudi hawakutaja kazi ya leo. Waliondolewa zaidi kutoka wakati wa sasa, na utengano wa muda wa zaidi ya miaka 4,000. Wala Yesu hakubashiri kikamilifu kazi ya leo, Akizungumzia kidogo tu, na bado mtu hupata ushahidi mchache. Ukilinganisha kazi ya leo na ya awali, zote mbili zinawezaje kulingana? Hatua ya kazi ya Yehova ilielekezwa kwa Israeli, hivyo ukilinganisha kazi ya leo nayo kutakuwa na hitilafu kubwa hata zaidi; hizo mbili haziwezi kulinganishwa kabisa. Wala wewe si wa Israeli, au Myahudi; uhodari wako na kila kitu kinachokuhusu kina upungufu—unawezaje kujilinganisha nao? Je, hii inawezekana? Jua kwamba leo ni Enzi ya Ufalme, na ni tofauti na Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kwa hali yoyote, usijaribu kutumia fomyula; Mungu hawezi kupatikana katika fomyula yoyote kama hiyo.
Yesu aliishije katika kipindi cha miaka 29 baada ya kuzaliwa Kwake? Biblia haina kumbukumbu yoyote ya utoto na ujana Wake; unajua yalivyokuwa? Inawezekana kuwa hakuwa na utoto au ujana, na kwamba alipozaliwa alikuwa tayari mwenye umri wa miaka 30? Unajua kidogo sana, hivyo usiwe mzembe unapotoa maoni yako. Haikupi faida! Biblia inarekodi tu kwamba kabla ya siku ya kuzaliwa ya 30, Yesu alibatizwa na Aliongozwa na Roho Mtakatifu kwenda jangwani kupitia jaribio la shetani. Na Injili Nne inarekodi kazi Yake ya miaka kumi na tatu na nusu. Hakuna rekodi ya utoto na ujana Wake, lakini hii haithibitishi kuwa Hakuwa na utoto na ujana; ni kwamba tu, mwanzoni, Hakufanya kazi yoyote, na Alikuwa mtu wa kawaida. Akiwa mtu wa kawaida, basi, Angeweza kuishi kwa miaka 33 bila ujana? Je, ingekuwa kuwa hakuwa na utoto? Je, Yeye angeweza kufikia ghafla umri wa miaka 33.5 bila kupitia umri wa 11 au 12, au 17 au 18? Kila kitu mtu anachofikiria juu Yake ni cha mwujiza. Mtu hana ukweli! Hakuna shaka kwamba Mungu mwenye mwili ana ubinadamu wa kawaida na wa desturi, lakini Anapotekeleza kazi Yake ni moja kwa moja na uungu Wake na ubinadamu usio kamili. Ni kwa sababu ya hili watu wana mashaka juu ya kazi ya leo, na hata juu ya kazi ya Yesu. Ingawa kazi ya Mungu inatofautiana katika mara mbili Anapokuwa mwili, dutu Yake haitofautiani. Bila shaka, ukisoma kumbukumbu za Injili Nne, tofauti ni kuu. Unawezaje kurudi kwenye maisha ya Yesu wakati wa utoto na ujana Wake? Unawezaje kuelewa ubinadamu wa kawaida wa Yesu? Labda una ufahamu thabiti wa ubinadamu wa Mungu leo, lakini hufahamu ubinadamu wa Yesu, hata zaidi hauuelewi. Isingeandikwa na Mathayo, usingekuwa na fununu ya ubinadamu wa Yesu. Labda, Nitakapokuambia kuhusu hadithi za Yesu wakati wa maisha Yake, na kukuambia ukweli wa ndani wa utoto na ujana wa Yesu, utatikisa kichwa chako: Hapana! Haiwezekani kuwa Alikuwa hivyo. Hawezi kuwa na udhaifu wowote, hata zaidi hapaswi kuwa na ubinadamu wowote! Hata utapaza sauti na kupiga yowe. Ni kwa sababu humjui Yesu kwamba una dhana juu Yangu. Unamwamini Yesu kuwa mwenye uungu pia, kuwa bila kitu cha mwili kumhusu. Lakini ukweli bado ni ukweli. Hakuna mtu anayetaka kuzungumza kinyume na ukweli wa ukweli, kwa maana Ninapozungumza ni kuhusiana na ukweli; sio bahatisho, wala si unabii. Jua kwamba Mungu anaweza kuinuka kwa kiwango kikubwa, na, zaidi ya hayo, Anaweza kujificha katika vina virefu. Yeye ni Asiyefikirika na akili yako, Yeye ni Mungu wa viumbe vyote, na sio Mungu binafsi ambaye Amedhaniwa na mtu mmoja hasa. Je, si hii ni sahihi?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumatatu, 3 Desemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake. Maana ya asili ya kushinda ni kuangamiza, kufedhehesha. Katika lugha Waisraeli walivyoeleza, ni kushinda kabisa, kuharibu, na kumfanya mwanadamu kutoweza kunipinga zaidi. Lakini leo kama linavyotumika kati yenu binadamu, maana yake ni kushinda. Mnapaswa kujua kwamba dhamira Yangu ni kuzima kabisa na kuangamiza yule mwovu kati ya binadamu, ili asiweze tena kuasi dhidi Yangu, sembuse kuwa na pumzi ya kupinga au kuleta fujo kwa Kazi Yangu. Hivyo, kulingana na wanadamu, imekuja kumaanisha kushinda. Haijalishi kidokezo cha neno hili, kazi Yangu ni kumshinda mwanadamu. Kwani. wakati ni ukweli kwamba mwanadamu ni kijalizo cha usimamizi Wangu, kwa usahihi zaidi, mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni yule mwovu anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo. Anga iliyo juu ya jamii ya binadamu ni nzito sana, ni yenye giza na huzuni, bila hata dalili ya uwazi, na ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, kiasi kwamba anayeishi ndani yake hawezi hata kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake au jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake, ni matope na imejaa mashimo makubwa, ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Na katika pembe zenye baridi na giza magenge ya mapepo yameshika makazi. Na kila mahali katika dunia ya binadamu, mapepo yanakuja na kwenda katika magenge. Kizazi cha wanyama wa aina yote, waliojawa na uchafu, wanapigana mkono kwa mkono katika mapambano ya kikatili, sauti ambayo huleta hofu moyoni. Nyakati kama hizo, katika dunia kama hiyo, “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kupata hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa tangu mwazo mwigizaji akitenda kwa mfano wa Shetani—hata zaidi, kuwa na mwili wake, wakitumika kama shahidi wa kushuhudia kwa Shetani, kwa uwazi. Aina hii ya jamii ya binadamu, aina hii ya watu wachafu walioharibika tabia, na watoto wa aina hii wa familia hii ya binadamu potovu, inawezaje kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Mtu anaweza kuanza wapi kuongea juu ya shahidi Wangu? Kwa adui ambaye, baada ya kupotosha mwanadamu, anasimama dhidi Yangu, tayari amemchukua mwanadamu—mwanadamu ambaye niliumba kitambo sana na ambaye alikuwa amejawa na utukufu Wangu kuishi kulingana na Mimi—na kumchafua. Amepokonya utukufu Wangu, na yote ambayo imetia moyoni mwa mwanadamu ni sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hapo mwanzo, Nilimuumba mwanadamu, yaani, Nilimuumba babu wa binadamu, Adamu. Alijaliwa na umbo na sura, mwenye kujawa na uhai, kujawa na nguvu ya maisha, na isitoshe, pamoja na utukufu Wangu. Hiyo ilikuwa ni siku tukufu Nilipomuumba mwanadamu. Baada ya hapo, Hawa alitengenezwa kutoka katika mwili wa Adamu, naye alikuwa pia babu wa binadamu, na hivyo watu niliowaumba walikuwa wamejazwa na pumzi Yangu na kujazwa na utukufu Wangu. Adamu kiasili aliumbwa kutoka kwa mkono Wangu na alikuwa akiwasilisha mfano Wangu. Hivyo maana ya asili ya “Adamu” ilikuwa kiumbe kilichoumbwa na Mimi, kilichojawa na nishati Yangu ya uhai, kilichojawa utukufu Wangu, kinacho sura na umbo, kinacho roho na pumzi. Alikuwa kiumbe wa pekee, aliyemilikiwa na roho, ambaye aliweza kuniwakilisha Mimi, kuwa na picha Yangu, na kupokea pumzi Yangu. Hapo mwanzo Hawa alikuwa mtu wa pili kujazwa na pumzi ambaye uumbaji wake nilikuwa nimeamuru, hivyo maana asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe ambaye angeendeleza utukufu Wangu, aliyejazwa na nguvu Zangu na zaidi ya hayo aliyejawa na utukufu Wangu. Hawa aliumbwa kutoka kwa Adamu, kwa hivyo alikuwa pia mfano Wangu, kwa maana yeye alikuwa mtu wa pili kuumbwa kwa mfano Wangu. Maana ya asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe hai, mwenye roho, mwili na mifupa, ushuhuda Wangu wa pili na pia mfano Wangu wa pili miongoni mwa mwanadamu. Walikuwa mababu wa wanadamu, hazina safi na ya thamani ya binadamu, na, kutoka awali, viumbe hai waliojaliwa na roho. Hata hivyo yule mwovu alikichukua kizazi cha mababu wa wanadamu na kukikanyaga na kukiteka nyara, kutosa ulimwengu wa binadamu katika giza totoro, na kuifanya kwamba kizazi chenyewe hakiamini tena katika uwepo Wangu. Kilicho cha chukizo zaidi ni kwamba, hata yule mwovu anapowapotosha watu na kuwakanyagia chini, anapokonya kwa ukatili utukufu Wangu, ushuhuda Wangu, nguvu Yangu Niliyowatolea watu, pumzi na maisha Niliyopuliza ndani yao, utukufu Wangu wote katika dunia ya binadamu, na damu yote ya roho ambayo nimetumia kwa mwanadamu. Mwanadamu hayupo tena katika mwanga, na amepoteza kila kitu Nilichompa, akiutupilia mbali utukufu ambao nimeutoa. Wanawezaje kukiri kwamba Mimi ndiye Bwana wa viumbe vyote? Wanawezaje kuendelea kuamini kuwepo Kwangu mbinguni? Wanawezaje kugundua udhihirisho wa utukufu Wangu duniani? Hawa wajukuu wa kiume na kike wanaweza kumchukua vipi Mungu ambaye mababu zao walimcha kama Bwana Aliyewaumba? Hawa wajukuu wenye kuhurumiwa “wamewasilisha” kwa ukarimu kwa yule mwovu utukufu, mfano, na vile vile ushahidi ambao Nilikuwa nimewatolea Adamu na Hawa, na pia maisha Niliyompa binadamu na ambayo ategemea ili kuwepo, na, bila kujali hata kidogo uwepo wa yule mwovu, amempa utukufu Wangu wote. Je, si hiki ni chanzo cha jina la “uchafu”? Jinsi gani aina hii ya mwanadamu , mapepo mabaya, aina hii ya maiti inayotembea, aina hii ya umbo la Shetani, na aina hii ya maadui Wangu zinaweza kumilikiwa na utukufu Wangu? Nitaumiliki tena utukufu Wangu, niumiliki ushuhuda Wangu ambao huwa miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyowahi kuwa mali Yangu na Nilivyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—nitamshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo, unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na dalili hata kidogo ya sumu yake. Na hivyo, Niliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kile kilichoumbwa na mkono Wangu, wale watakatifu ambao nawapenda na wasio wa mwingine yeyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu cha asili tena. Kwa sababu Ninanuia kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika kumshinda Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kusudi la starehe Yangu. Haya ndiyo mapenzi Yangu.
Mwanadamu ameendelea kwa makumi ya maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia alipo leo. Hata hivyo, mwanadamu wa uumbaji Wangu wa asili kwa muda mrefu uliopita amezama katika upotovu. Tayari amecha kuwa kile Ninachotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, hawastahili tena jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, ambao Shetani amewateka nyara, maiti zilizooza zinazotembea ambamo Shetani huishi na huvalia. Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuja Kwangu. Mwanadamu kwa shingo upande tu huyajibu maombi Yangu, na kwa muda anakubaliana nayo, na hashiriki kwa kweli katika furaha na huzuni za maisha pamoja na Mimi. Kwa vile wanadamu huniona Mimi kama Asiyeeleweka, bila ya kutaka wao hujifanya wanatabasamu Kwangu, kuleta namna ya kujidekeza kwa yule aliye na madaraka. Hii ni kwa sababu watu hawana ufahamu wa kazi Yangu, sembuse mapenzi Yangu kwa wakati wa sasa. Nitakuwa wazi na nyinyi nyote: Siku itakapofika, mateso ya mwanadamu yeyote ambaye huniabudu yatakuwa rahisi kubeba kuliko yenu. Kiwango cha imani yenu Kwangu hakiwezi, kwa hakika, kuzidi kile cha Ayubu—hata imani ya Mafarisayo Wayahudi inaishinda yenu—na hivyo, siku ya moto ikifika, kuteseka kwenu kutakuwa kali zaidi kuliko kule kwa Mafarisayo walipokemewa na Yesu, kuliko kwa wale viongozi 250 waliompinga Musa, na kuliko kulw kwa Sodoma chini ya moto mkali wa uharibifu wake. Musa alipougonga mwamba, na maji yaliyokuwa yametolewa na Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza kinubi kwa kunisifu Mimi, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake waliojaa kote milimani na mali nyingi sana, na mwili wake kujawa na majipu mabaya, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Sababu ya yanayodaiwa kuwa mataifa mengi yasiyo ya Kiyahudi kupata ufunuo Wangu, na yakajua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Je si wote ambao wamepigwa na maneno Yangu makali na bado wanafarijiwa nayo, na ambao wameokoka—wamefanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Wale wanaoamini Kwangu lakini bado hupitia mateso, je si pia wamekataliwa na dunia? Wale wanaoishi nje ya neno Langu, wakikimbia mateso ya majaribu, si wao wote wanazurura tu ulimwengu? Wao ni sawa na majani ya msimu wa kupukutika kwa majani yanayopeperuka hapa na pale, bila pahali pa kupumzika, sembuse neno Langu la kufutia machozi. Ingawa adabu na usafishaji wangu hauwafuati wao, je, wao si waombaji, wanaoelea kila mahali, ambao wakitangatanga katika mitaa iliyo nje ya Ufalme wa mbinguni? Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli? Je, unaweza kweli kupata tabasamu hata dhaifu ya kutosheleza kutoka kwa dunia kwa kuepuka adabu yangu? Je, unaweza kweli kutumia starehe zako za kidunia kuficha utupu ulio katika moyo wako usioweza kufichika? Unaweza kumdanganya mtu yeyote katika familia yako, ilhali huwezi kunidanganya Mimi kamwe. Kwa kuwa imani yako ni ndogo sana, mpaka wa leo huna uwezo wa kupata raha inayoletwa na maisha. Nakushauri: heri kutumia nusu ya maisha yako kwa ajili Yangu kwa dhati kuliko kuishi maisha yako yote katika hali hafifu na kujishughulisha kwa ajili ya mwili, kuvumilia mateso yote ambayo ni vigumu binadamu kuvumilia. Kuna faida gani ya wewe kujipenda sana na kuikimbia adabu Yangu? Kuna faida gani wewe kujificha kutoka kwa adabu Yangu ya muda mfupi tu, na mwishowe kupate aibu ya milele, na adabu ya milele? Mimi, kwa hakika, Simlazimishi yeyote kufanya mapenzi Yangu. Iwapo mtu kweli anayo nia ya kujiwasilisha kwa mipango Yangu yote, Sitamtendea vibaya. Lakini Nahitaji kwamba watu wote waamini ndani Yangu, kama vile Ayubu alivyoamini ndani Yangu, Yehova. Iwapo imani yenu inazidi ile ya Tomaso, basi imani yenu itapata pongezi Zangu, katika uaminifu wenu mtapata furaha Yangu, na hakika mtapata utukufu Wangu katika siku zenu. Hata hivyo, watu, wanaoamini katika dunia na wanaomwamini ibilisi, wamefanya mioyo yao kuwa migumu, kama vile halaiki za mji wa Sodoma, na chembe za mchanga zilizovumwa na upepo katika macho yao na sadaka kutoka kwa ibilisi zikiwa zimeshikiliwa vinywani mwao, akili zao zilizodanganywa tangu kitambo zimemilikiwa na yule mwovu ambaye ameipora dunia. Mawazo yao nusura yameporwa na ibilisi wa nyakati za kale. Na hivyo, imani ya mwanadamu imekwenda na upepo, na hawezi hata kuitambua Kazi Yangu. Anachoweza tu kufanya ni kujaribu nkwa unyonge kuvumilia au kuchambua kwa kukisia sana, kwa sababu kwa muda mrefu tayari amejawa na sumu ya Shetani.
Mimi Nitawashinda wanadamu kwa sababu wanadanu waliumbwa na Mimi wakati mmoja na pia, kilicho cha ziada, wamefurahia vitu vyote karimu vya uumbaji Wangu. Lakini wanadamu pia wamenikataa Mimi, na nyoyo zao haziko na Mimi ndani yao, na wao huniona kama mzigo kwa uwepo wao, hadi kwa kiwango ambacho, wakiwa kwa kweli wameniona, watu bado wananikataa, na kukuna vichwa wakiwaza kila njia inayoweza kuwawezesha kunishinda Mimi. Watu huwa hawaniruhusu Mimi kuwachukulia kwa umakini au kuweka madai kali juu yao, wala hawanikubali huhukumu au kuadibu udhalimu wao. mbali na kuona hili kuwa jambo la kuvutia, wanakasirika. Na hivyo Kazi Yangu ni kuchukua mwanadamu ambaye hula, hunywa na kusherehekea Kwangu lakini hanijui na kumshinda. Nitawapokonya zana wanadamu, na kisha, Nikiwachukua malaika Wangu, Nikiuchukua utukufu Wangu Nitarejea kwenye makao Yangu. Kwa kuwa kile ambacho watu wamefanya kimenivunja moyo kabisa na kuitawanya kazi Yangu kwa vipande muda mrefu uliopita. Nanuia kuumiliki tena utukufu ambao yule mwovu ameiba kabla ya kuondoka kwa furaha, na kuwaacha wanadamu waendelee kuishi maisha yao, waendelee na “kuishi na kufanya kazi kwa amani na furaha,” na Mimi sitaingilia kati tena katika maisha yao. Lakini Mimi sasa Nanuia kikamilifu kuumiliki tena utukufu Wangu kutoka kwa mkono wa yule mwovu, kuurejesha ukamilifu wa utukufu Niliouumba ndani ya mwanadamu wakati wa kuumbwa kwa dunia, na kamwe tena kutotolea mwanadamu wa dunia. Kwa kuwa wanadamu hawajashindwa tu kuuhifadhi utukufu Wangu, bali pia wao wameugeuza kuwa mfano wa Shetani. Watu hawathamini kuja Kwangu, wala hawaiwekei thamani siku ya utukufu Wangu. Wao hawasherehekei kupokea adabu Yangu, sembuse kuwa tayari kuurejesha utukufu Wangu Kwangu. Wala hawako tayari kutupa mbali sumu ya yule mwovu. Wanadamu bado siku zote wananidanganya kwa njia ile ile ya zamani, bado wakivaa tabasamu za kung’aa na nyuso zenye furaha kwa njia ile ile ya zamani. Wao hawajui kina cha huzuni ambayo wanadamu watakabiliwa nao baada ya utukufu Wangu kuwaondoka, na hasa hawajui kwamba siku Yangu itakapokuja kwa wanadamu wote, watakuwa na wakati hata mgumu zaidi kuliko watu katika nyakati za Nuhu. Kwa maana wao hawajui giza iliyokuwepo Israeli wakati utukufu Wangu ulitoweka kwa kuwa mwanadamu husahau kunapokucha jinsi ilivyokuwa vigumu kupita katika giza la usiku wa manane. Jua linaporejea mafichoni tena na giza kumshukia mwanadamu, ataanza tena kuomboleza na kusaga meno yake gizani. Je, mmesahau, wakati utukufu Wangu ulipotoweka kutoka Israeli, ilivyokuwa vigumu kwa watu wake kuishi siku zao za mateso? Huu ndio wakati ambapo mnaona utukufu Wangu, na pia ndio wakati ambapo mnashiriki siku ya utukufu Wangu. Mwanadamu ataomboleza katikati ya giza wakati utukufu Wangu unapoondoka kutoka katika nchi chafu. Sasa ndio siku ya utukufu Ninapofanya kazi Yangu, na pia ndio siku ambapo Namwondoa mwanadamu kutoka kwa mateso, kwa kuwa sitapitia nyakati za uchungu na ugumu nao. Mimi Nataka tu ushindi kamili juu ya wanadamu na kumshinda kikamilifu yule mwovu wa wanadamu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Jumapili, 2 Desemba 2018

Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?" (Official Video)

Neno la Mungu "Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?" (Official Video)

Mwenyezi Mungu anasema, "Unapaswa kuona kuwa mapenzi Yake na kazi Yake si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Kwa sababu kazi ya leo ni kubadilisha wale waliopotoshwa, wale waliokufa ganzi, na kutakasa walioumbwa kisha kushughulikiwa na Shetani, si kuumba Adamu na Hawa, ama hata kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayvodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake."
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumamosi, 1 Desemba 2018

Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, sauti ya Mungu

Mtu Ambaye Hupata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Radhi Kutenda Ukweli

Hapo awali sana, umuhimu wa kuwa na maisha sahihi ya kanisa ulitajwa katika mahubiri. Kwa hivyo ni kwa nini maisha ya kanisa hayajaboreka bado, na bado ni kile kitu kimoja tu cha zamani? Mbona hakuna njia mpya na tofauti kabisa ya maisha? Je, inaweza kuwa sahihi kwa mtu wa miaka ya tisini kuishi kama mfalme wa enzi iliyopita? Ingawa chakula na vinywaji vinaweza kuwa vyakula vitamu vilivyoonjwa mara chache katika enzi zilizopita, hapajakuwa na mabadiliko makubwa katika hali kanisani. Imekuwa kama kuweka divai ya kale katika kiriba kipya. Je, kuna haja gani basi ya Mungu kusema sana? Makanisa katika maeneo mengi hayajabadilika kabisa. Mimi nimeliona kwa macho Yangu na ni wazi katika moyo Wangu; Hata kama sijapata uzoefu wa maisha ya kanisa Mimi Mwenyewe, Nazijua hali za mikusanyiko ya kanisa kama mgongo wa mkono Wangu. Hawajafanya maendeleo mengi. Inarejelea msemo—ni kama kutia divai ya kale katika kiriba kipya. Hakuna kilichobadilika, siyo hata kidogo! Wakati mtu anapowachunga wao huwaka kama moto, lakini wakati hakuna mtu hapo kuwafadhili, wao ni kama pande kubwa la barafu. Si wengi wanaoweza kuzungumza juu ya mambo ya vitendo, na ni mara chache mtu yeyote anaweza kushika usukani. Ingawa mahubiri ni ya juu, imekuwa nadra kwa mtu yeyote kupata kuingia. Watu wachache hutunza neno la Mungu. Wao hujawa na machozi wanapolikubali neno la Mungu na kuwa wachangamfu wanapoliweka kando; Wao husononeka na kuwa wenye huzuni wanapoliondokea. Kwa kusema kweli, nyinyi hamlitunzi neno la Mungu, na hamyaoni kamwe maneno kutoka kinywa Chake mwenyewe kama hazina. Nyinyi huwa na wasiwasi tu mnapolisoma neno Lake, na kuhisi ni lenye kuhitaji nguvu nyingi sana mnapolikariri, na inapofika kuliweka neno Lake katika matendo, ni kama kukabiliana na kazi isiyoweza kukamilika—hamjamotishwa, Nyinyi daima huwa mnachangamka mnaposoma neno la Mungu, lakini mnasahau mnapolitenda. Kwa hakika, maneno haya si lazima yazungumzwe kwa jitihada sana na kurudiwa kwa uvumilivu sana; watu husikiliza tu lakini hawayaweki katika matendo, kwa hiyo kimekuwa kizuizi kwa kazi ya Mungu. Mimi siwezi kukosa kulileta jambo hili kwa mjadala, Mimi siwezi kukosa kulizungumzia. Mimi ninalazimika kufanya hivyo; Siyo kwamba Mimi hufurahia kufunua udhaifu wa wengine. Mnafikiri kwamba matendo yenu yanafaa tu na mnadhani kwamba wakati ufunuo uko kileleni, kwamba mmeingia katika kilele pia? Je, ni rahisi hivyo? Hamchunguzi kamwe msingi ambao uzoefu wenu hatimaye umejengwa juu yake. Kwa wakati huu, mikusanyiko yenu haiwezi kuitwa maisha mazuri ya kanisa kabisa, wala kuwa maisha yafaayo ya kiroho kamwe. Ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao hufurahia kuzungumza na kuimba. Kusema kweli, hakuna uhalisi mwingi ndani yake. Kulisema kwa dhahiri zaidi, kama hutendi, u wapi uhalisi? Je, huko siko kujigamba kusema kwamba una uhalisi? Wale ambao daima hufanya kazi ni wa kujigamba na wenye majivuno, wakati ambapo wale ambao hutii daima hutulia na kuinamisha vichwa vyao chini, bila nafasi yoyote ya kutenda. Watu ambao hufanya kazi huwa hawafanyi chochote ila kuzungumza, kuendelea zaidi na zaidi na mazungumzo yao yenye kuvutia, na wafuasi husikiliza tu. Hakuna mabadiliko ya kuzungumzia; Hizi ni njia tu za zamani! Leo, kuweza kwako kunyenyekea na kutothubutu kuingilia au kutenda makusudi ni kutokana na kuwasili kwa amri za kiutawala za Mungu; siyo mabadiliko uliyoyapata kupitia uzoefu. Ukweli kwamba kuna mambo mengi ambayo huwezi kuyafanya leo ambayo ungeweza kuyafanya jana ni kwa sababu kazi ya Mungu ni dhahiri kiasi kwamba imeshinda watu. Acha Nimuulize mtu fulani, ni kiasi gani cha ufanikishaji wako leo kilichopatikana kwa jasho la kazi ngumu yako mwenyewe? Ni kiasi gani ulichoambiwa moja kwa moja na Mungu? Ungejibu vipi? Je, ungepigwa na bumbuwazi na kutoweza kunena? Ungekosa adabu? Ni kwa nini wengine wanaweza kuzungumza juu ya mengi ya uzoefu wao ili kukuruzuku, wakati ambapo unafurahia tu chakula ambacho wengine wamepika? Je, huoni haya? Je, hutahayari?
Mnaweza kutekeleza uchunguzi wa kutafuta ukweli, kuchunguza wale walio katika viwango vya juu ambao yamkini ni bora zaidi: Unaelewa ukweli kiasi gani? Je, ni kiasi gani ambacho wewe hatimaye huweka katika mazoezi? Ni nani unayempenda zaidi, Mungu au wewe mwenyewe? Je, wewe hutoa mara nyingi zaidi, au hupokea mara nyingi zaidi? Je, ni mara ngapi wakati lengo lako lilikuwa lenye kosa umetelekeza nafsi yako ya zamani na kuyaridhisha mapenzi ya Mungu? Maswali haya machache tu yatawakanganya watu wengi. Kwa watu wengi sana, hata kama wakitambua kuwa nia yao si sahihi, bado hufanya makosa makusudi, nao hata hawajakaribia kuinyima miili yao wenyewe. Watu wengi sana huruhusu dhambi kuenea kote ndani yao, wakiruhusu hali ya dhambi kuongoza kila tendo lao. Hawawezi kushinda dhambi zao, na huendelea kuishi katika dhambi. Baada ya kufika kwenye hatua hii ya sasa, ni nani asiyejua ni matendo mangapi mabaya ameyafanya? Ukisema hujui, basi Mimi ningesema kwamba unasema uongo. Kusema ukweli, yote ni kutotaka kutelekeza nafsi yako ya zamani. Je, kuna maana gani ya kusema "maneno mengi kutoka kwa moyo" ya kutubu ambayo hayafai? Je, hili lingekusaidia kukua katika maisha yako? Kujijua mwenyewe ni kazi yako ya kudumu. Mimi huwafanya watu wakamilifu kupitia utii wao na kutenda kwao kwa maneno ya Mungu. Ukivaa tu neno la Mungu kama jinsi ungevaa nguo zako, ili kuwa tu nadhifu na maridadi, je, hujidanganyi mwenyewe na kuwadanganya wengine? Ikiwa yote uliyonayo ni kuongea na kamwe huyaweki katika matendo, ni kitu gani utakachokifikia?
Watu wengi wanaweza kuzungumza kidogo juu ya matendo na wanaweza kuzungumza kuhusu fikira zao za kibinafsi, lakini mengi yayo ni mwanga kutoka kwa maneno ya wengine. Haijumuishi chochote kutoka kwa matendo yao binafsi kamwe, wala kujumuisha kile wanachokiona kutokana na uzoefu wao. Nimechangua suala hili mapema; usifikiri kwamba sijui chochote. Wewe ni tishio la bure tu, na bado unaongea juu ya kumshinda Shetani, juu ya kutoa ushahidi wa ushindi, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa Mungu? Huu wote ni upuuzi! Je, unadhani kwamba maneno yote ambayo Mungu ameyasema leo ni yako kupendezwa nayo? Kinywa chako hunena juu ya kutelekeza nafsi yako ya zamani na kuweka ukweli katika matendo, lakini mikono yako inafanya vitendo vingine na moyo wako unapanga hila zingine—wewe ni mtu wa aina gani? Kwa nini moyo wako na mikono yako si kitu kimoja? Kuhubiri kwingi sana kumekuwa maneno matupu; si hili ni la kuvunja moyo? Ikiwa umeshindwa kuweka neno la Mungu katika matendo, inathibitisha kuwa bado hujaingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi, bado haujapata kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako, na bado haujapata mwongozo Wake. Ukisema kuwa unaweza tu kuelewa neno la Mungu lakini umeshindwa kuliweka katika matendo, basi wewe ni mtu asiyependa ukweli. Mungu huwa haji kumwokoa mtu wa aina hii. Yesu alipatwa na maumivu makubwa wakati Yeye aliposulubiwa ili kuwaokoa wenye dhambi, kuwaokoa maskini, kuwaokoa hao watu wanyenyekevu. Kusulubiwa Kwake kulileta sadaka ya dhambi. Ikiwa huwezi kutenda neno la Mungu, basi unapaswa kuondoka haraka unavyoweza; usijikalie pote katika nyumba ya Mungu kama doezi. Watu wengi hata huona vigumu kujizuia kufanya mambo ambayo humpinga Mungu kwa dhahiri. Je, si wanauliza kifo? Wanawezaje kuongea juu ya kuingia katika ufalme wa Mungu? Je, wangekuwa na ujasiri wa kuuona uso Wake? Kula chakula ambacho Yeye hukupa, kufanya mambo ya uhalifu ambayo humpinga Mungu, kuwa mwenye nia mbaya, mwenye kudhuru, na mwenye hila, hata wakati Mungu anakuruhusu kufurahia baraka ambazo Yeye amekupa—je, huzihisi zikiichoma mikono yako unapozipokea? Je, huuhisi uso wako ukigeuka kuwa mwekundu? Baada ya kufanya kitu kinyume na Mungu, baada ya kufanya hila ili "kuwa laghai," huhisi hofu? Kama huhisi chochote, unawezaje kuzungumza juu ya wakati wowote ujao? Kulikuwa tayari hakuna wakati ujao kwako zamani za kale, kwa hiyo ni matarajio yapi makubwa zaidi unaweza kuwa nayo bado? Ukisema kitu bila haya lakini huhisi hatia, na moyo wako hauna ufahamu, basi haimaanishi kwamba tayari umekataliwa na Mungu? Kuzungumza na kutenda kwa kujiachia na bila kuzuiwa imekuwa asili yako; Je, unawezaje kufanywa mkamilifu na Mungu hivi? Ungeweza kutembea ulimwenguni kote? Ni nani angethibitishiwa na wewe? Wale ambao wanaijua asili yako ya kweli watakaa mbali nawe. Je, si hii ni adhabu ya Mungu? Kwa jumla, ikiwa kuna mazungumzo tu bila matendo, hakuna ukuaji. Ingawa Roho Mtakatifu anaweza kuwa anafanya kazi kwako unapozungumza, kama hutendi, Roho Mtakatifu ataacha kufanya kazi. Ukizidi kuendelea kwa njia hii, kunawezaje kuwa na majadiliano yoyote ya wakati ujao au kutoa nafsi yako yote kwa kazi ya Mungu? Wewe husema tu juu ya kutoa nafsi yako yote, na bado humpi Mungu moyo wako ambao kwa hakika humpenda Yeye. Yote ambayo Mungu amepokea ni moyo wa maneno yako, na siyo moyo wa utendaji wako. Je, hiki kinaweza kuwa ndicho kimo chako cha kweli? Ikiwa ungeendelea kwa jinsi hii, ungefanywa mkamilifu na Mungu lini? Je, huhisi wasiwasi juu ya kesho yako ya giza na majonzi? Je, huhisi kwamba Mungu amepoteza tumaini kwako? Je, hujui kwamba Mungu hutamani kuwapa ukamilisho watu wengi na wapya? Je, vitu vya zamani vingeweza kukacha? Wewe huyazingatii maneno ya Mungu leo: Je, unasubiri kesho?
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. ... Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka."

Alhamisi, 29 Novemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake."
Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri shahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji tukufu wa Bwana Yesu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunawaza kuhusu haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa tulizaliwa nyakati za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya malipo ya “utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa”; hii ni baraka iliyoje! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja kila mara. Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema wakati mwanadamu hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na atatokea kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja ya wale watakaochukuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine wameachana na familia zao, wengine kukana ndoa zao, na baadhi yao hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anavyompa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, na matumizi yetu, tunaamini, tayari yametazamika machoni pake. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi Zake kutoka kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Pia, bila kusita hata kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu kinachotarajiwa.
kutoka kwa Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Jumatano, 28 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wimbo wa Kifuasi cha Dhati

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, nyimbo za injili

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wimbo wa Kifuasi cha Dhati

I
Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili. Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli. Hekima Yake, Uadilifu Wake, nayapenda yote. Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana. Kuna Mmoja hapa, Yeye ni Mungu katika mwili. Anayoyasema, Anayoyafanya, yote ni ukweli. Hekima Yake, uadilifu Wake, nayapenda yote. Kukutana Naye, kumpata Yeye, nimebarikiwa sana. Moyo wake, Upendo wake, vimefanya nishindwe. Mpe upendo, mfuate Yeye, ah mpendwa wangu. Nampenda, najihisi mtamu, teseka kwa ajili Yake. Mpate, ishi kwa ajili Yake, mpende milele.
II
Moyo wangu, Alioupewa, nahisi furaha. Nafsi yangu nzima kuishi kwa ajili Yake, haya ni maisha yangu. Kumpenda, kumtumikia, heshima kubwa kwangu. Moyo wangu hautaki kingine chochote, nimetosheka. Yajali mapenzi Yake, fikra zake, na mahangaiko Yake. Ni mapenzi yangu kumpendeza na kumtosheleza Mungu. Mimi huhudumu katika nyumba ya Mungu, nikitimiza wajibu. Humtii, kuwa mwaminifu kwake, na kujitolea. Moyo wake, Upendo wake, vimefanya nishindwe. Mpe upendo, mfuate Yeye, ah mpendwa wangu. Nampenda, najihisi mtamu, nateseka kwa ajili Yake. Mpate, ishi kwa ajili Yake, mpende milele.
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Soma Zaidi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumanne, 27 Novemba 2018

Swahili Christian Song "Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu" | The Lord Has Come Back (Tai Chi Dance)

Swahili Christian Song "Umuhimu wa Kuonekana kwa Mungu" | The Lord Has Come Back (Tai Chi Dance)

Kuonekana kwa Mungu kunataja kufika Kwake binafsi duniani ili kufanya kazi Yake. Na utambulisho Wake mwenyewe na tabia, na kwa njia Yake mwenyewe, Yeye anashuka kati ya mwanadamu ili kuanza enzi na kumaliza enzi. Kuonekana kama huku sio ishara ama picha. Si aina ya sherehe. Si muujiza. Si ono kuu. Pia sio aina ya mchakato wa kidini hata zaidi. Ni ukweli halisi ambao unaweza kuguswa na kuonwa, ukweli ambao unaweza kuguswa na kuonwa. Konekana kama huku sio kwa ajili ya kufuata mchakato, ama kwa ajili ya shughuli ya muda mfupi; lakini ni, kwa ajili ya hatua ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu.
Kuonekana kwa Mungu kila mara ni kwa maana, na kuna uhusiano na mpango Wake wa usimamizi, kuna uhusiano na mpango Wake wa usimamizi. Konekana huku si sawa kabisa na kuonekana kwa Mungu akiongoza mwanadamu, kumwongoza mwanadamu au kumtia nuru mwanadamu, kumwongoza mwanadamu au kumtia nuru mwanadamu. Mungu anafanya hatua ya kazi kuu kila wakati Anapojifichua Mwenyewe. Kazi hii ni tofauti na ile ya enzi nyingine yoyote, isiyoweza kufikiriwa na mwanadamu, haijapitiwa na mwanadamu kamwe, haijapitiwa na mwanadamu kamwe. Ni kazi inayoanzisha enzi mpya na kumaliza enzi nzee, kazi mpya na bora ya wokovu wa binadamu, na kazi ya kumleta binadamu katika enzi mpya. Ni umuhimu wa kuonekana kwa Mungu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?